Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwili wa Raila Odinga Wawasili Nchini Kenya, Wapokelewa na Rais Ruto JKIA

  • 6
Scroll Down To Discover

Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, umewasili nchini Kenya leo asubuhi kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), ukitokea nchini India ambako alikuwa akipokea matibabu.

Rais wa Kenya William Ruto, pamoja na Rais wa zamani Uhuru Kenyatta, familia ya Raila Odinga, na viongozi wakuu wa serikali, wameongoza mapokezi hayo rasmi uwanjani.

Ujumbe maalum kutoka Kenya ulitumwa jana kwenda India kuchukua mwili wa kiongozi huyo mkongwe wa kisiasa, ambaye amekuwa nguzo muhimu katika historia ya demokrasia nchini humo.

Baada ya mapokezi, mwili huo umepelekwa Lee Funeral Home, jijini Nairobi, kwa maandalizi ya taratibu za mazishi.



Prev Post Waziri Mkuu Majaliwa Mgeni Rasmi Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Chakula
Next Post Jeshi la Ulinzi la Wananchi latoa tamko kuhusu uchaguzi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook