Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia Aahidi Uwanja wa Ndege Mpya Kagera, Kuchochea Utalii na Biashara

  • 3
Scroll Down To Discover

MISENYI, KAGERA — Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa katika eneo la Kyabajwa, wilayani Misenyi, mkoani Kagera, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.

Akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kyaka, Dkt. Samia alisema serikali yake imeanza hatua za upembuzi yakinifu kwa ajili ya kujenga uwanja huo utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa za kimataifa ikiwemo Boeing 737-900, zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 180 hadi 220.

“Tumeanza kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa katika eneo la Kyabajwa. Awali, ilipendekezwa Omukajunguti, lakini eneo hilo halikufaulu vizuri katika upembuzi yakinifu, hivyo tumeamua kujenga Kyabajwa,” alisema Dkt. Samia.

Rais Samia alisisitiza kuwa mradi huo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu ya usafiri na kusukuma mbele sera ya kilimo biashara, kwa kuwezesha usafirishaji wa mazao na bidhaa za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Ameeleza kuwa uwanja huo wa ndege utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Kagera na maeneo jirani, hususan katika sekta za utalii, kilimo, na biashara ya mipakani.

“Uwanja huu utasaidia kufungua milango ya fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Misenyi na maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Uganda. Ni hatua muhimu kuelekea Kagera mpya yenye uchumi imara na ushindani wa kikanda,” aliongeza.

Uwanja wa ndege wa Kyabajwa unatarajiwa kuwa miongoni mwa viwanja vikubwa vya kisasa nchini, ukiwa na miundombinu itakayowezesha ndege kubwa kutua na kuruka kwa usalama, pamoja na huduma za abiria na mizigo za kimataifa.

Mradi huu unatajwa kuwa chachu ya kukuza uwekezaji, ajira, na utalii katika mkoa wa Kagera, na unalenga kubadilisha taswira ya usafiri wa anga katika Kanda ya Ziwa.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 16, 2925
Next Post Watuhumiwa 17 Mbaroni Kwa Wizi Wa Pikipiki Zanzibar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook