Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Uwanja wa Sokoine Wafungwa Kutumika Kwa Mechi za Ligi

  • 2
Scroll Down To Discover

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa Sokoine uliopo jijini Mbeya kutumika kwa michezo ya Ligi, kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni na masharti ya sheria za mpira wa miguu.

TFF imesema miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni za Leseni za Klabu, kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni hizo.

Kutokana na uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kuutumia uwanja mwingine kwa mujibu wa Kanuni, hadi pale marekebisho yatakapokamilika na ukaguzi kufanywa upya na TFF.

TFF imezikumbusha klabu zote nchini kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja vyao ili viendelee kukidhi viwango vinavyotakiwa.



Prev Post Kesi ya Luhaga Mpina Yatupiliwa Mbali, NEC Yapewa Uhalali wa Maamuzi Yake
Next Post Walimu Kutoka Taasisi Ya Henan Polytechnic (Hpi) Ya China Watoa Mafunzo Kipawa Chini Ya Mradi Wa Zhangheng
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook