Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wenje Ampongeza Dkt. Samia kwa Mapinduzi ya Sheria – Video

  • 2
Scroll Down To Discover

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya ziwa Victoria na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, ambaye kwasasa ni Mwanachama na Kada Mtiifu wa CCM, Ndugu. Ezekiel Wenje

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya ziwa Victoria na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, ambaye kwasasa ni Mwanachama na Kada Mtiifu wa CCM, Ndugu. Ezekiel Wenje amesema ni hatari kwa Taifa kuwa na Kiongozi mkubwa wa Chama Cha Siasa anayesema kuwa yupo tayari kufa huku akibainisha kuwa CHADEMA ilijiondoa kwenye Uchaguzi kwa hiari yao wenyewe kutokana na uoga na kuogopa ushindani uliopo kwenye Uchaguzi nchini Tanzania.

Ndg. Wenje ameyasema hayo mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa Muleba alipopewa nafasi hiyo kwenye Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kupitia CCM ndani ya mkoa wa Kagera kwenye Viwanja vya CCM Zimbihile, leo tarehe 15 Oktoba 2025.

Mbele ya kadamnasi hiyo, Ndg. Wenje amesema hatua ya CHADEMA kususia uchaguzi ilifanyika licha ya mapendekezo yao yote waliyoyawasilisha kwa Serikali ya awamu ya sita kuwa yamefanyiwa kazi.

“Biblia inasema Mungu hafanyi kazi na watu waoga wanaoogopa ushindani.”

“Sasa watu waoga wanaokimbia uchaguzi licha ya mapendekezo na maombi yao kufanyiwa kazi ni hodari na shujaa?”

“..Ni hatari sana kuwa na Kiongozi wa Chama Cha Siasa anayesema yupo tayari kufa. Kiongozi aliye tayari kufa ni Kiongozi aliyekata tamaa kwasababu hakuna matumaini kwenye kifo.”

Akipongeza kubwa ya Dkt. Samia katika miaka 4 iiyopita, Ndg. Wenje ametoa shukrani Dkt. Samia kwa utekelezaji wa mapendekezo mbalimbali ya mifumo na sheria za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kupenda kwake maridhiano na mazungumzo na makundi mbalimbali ya Kijamii na kisiasa kama ambavyo CHADEMA ilikuwa ikiitwa mara kadhaa Ikulu na Rais Samia na badala yake Chama hicho kikawa kinasusa kukutana naye.

Vilevile, amempingeza Dkt. Samia kwa kufungulia mikutano ya hadhara pamoja na mabadiliko ya sheria za uchaguzi ikiwemo kutaka marekebisho ya kuzuia Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi Mkuu pamoja na kufuta kipengele cha kupita bila kupingwa.



Prev Post Dkt. Samia: Serikali Italipa Kipaumbele Zao la Vanila na Miundombinu Kagera
Next Post Watu Wanne Wakamatwa Dar kwa Kumiliki Vyombo vya Habari Bila Leseni – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook