Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Imeweka Mikakati Dhabiti Ya Kukabiliana Na Majanga Nchini-Majaliwa

  • 8
Scroll Down To Discover


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha ustahimilivu wa Taifa dhidi ya majanga, kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati na miradi mbalimbali

Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuendelea katika kujenga ustahimilivu wa jamii dhidi ya maafa, tutaokoa maisha, mali, na rasilimali za taifa letu.

Amesema hayo leo Jumatatu (Oktoba 13, 2025) wakati alipotoa tamko katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupunguza madhara ya maafa, katika ukumbi wa mikutano wa City Park Garden jijini Mbeya.

Akitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imeandaa na kuhuisha nyaraka za kitaifa kuhusu maafa ikiwemo Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa (toleo la 2025), Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022–2027) na Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa (2022).

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hatua nyingine ni Kuimarisha usahihi wa utabiri wa hali ya hewa kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), ambao sasa umefikia asilimia 85, hivyo kusaidia kupunguza madhara ya maafa kwa zaidi ya asilimia 30.

“Pia Serikali time inatosha mifumo ya tahadhari ya mapema kwa kuwezesha vifaa na teknolojia za kisasa, ikiwemo kuanzishwa kwa Kituo cha Ufuatiliaji wa Majanga na Utoaji wa Taarifa za Tahadhari kilichounganishwa na vituo vya kikanda barani Afrika”.

Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa yenye kuzingatia ustahimilivu wa tabianchi ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Kidunda wenye thamani ya shilingi bilioni 329.47, Bwawa la Farkwa wenye thamani ya shilingi bilioni 312.08 pamoja na Mradi wa Maji Ziwa Victoria-Simiyu wenye thamani ya bilioni 440.

Katika Sekta ya Kilimo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendeleza mbinu za ustahimilivu kwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, mbegu bora, mifumo ya tahadhari mapema, na ushirikiano na wakulima wadogo.

“Aidha, Serikali imeendelea kulijengea uwezo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwezesha vifaa, teknolojia, na mafunzo ya kisasa ili kuboresha huduma za uokozi na uzimaji moto”

Pia Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika uwekezaji unaozingatia ustahimilivu dhidi ya majanga, ikiwemo uwekaji wa bima na utekelezaji wa miongozo ya Serikali.

Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi amesema kuwa maadhimisho haya yana lengo la kuhamasisha ushiriki wa wadau wote katika shughuli zausimamizi wa maafa.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kuratibu utoaji mafunzo kwa wataalamu wa sekta, mikoa na jamii wakiwemovijana kuhusu usimamizi wa maafa hususanikatika hatua za kuzuia na kujiandaa kukabilimaafa yanapotokea pamoja na kurejesha hali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa Sandra Hakim amesema kuwa wadau mbalimbali ikiwemo Watendaji wa Serikali za Mitaa, Viongozi wa kijamii, Asasi za Kiraia pamoja, Umoja wa Mataifa na mashirika ya Kimataifa wamekuwa wakifanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali kwenye majanga.

Awali Mheshimiwa Majaliwa alikagua maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru Pamoja na kumbukizi ya baba wa Taifa itakayofanyika katika uwanja wa CCM Sokoine jijini Mbeya.



Prev Post Umati wa Wananchi wa Katoro Wampongeza Dkt. Samia Katika Mkutano wa Kampeni – Picha
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook