Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kampuni Ya Kijiji Kwa Kijiji Jimbo La Musoma Vijijini

  • 6
Scroll Down To Discover

Musoma Vijijini, Oktoba 12, 2025
Madiwani kupitia Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameungana na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, katika harakati za kusaka kura kupitia kampeni ya mafiga matatu Rais, Mbunge na Madiwani.

Wakihutubia wananchi katika mikutano ya kampeni iliyofanyika leo katika vijiji vya Kwikuba (Kata ya Busambara) na Nyang’oma (Kata ya Mugango), madiwani hao wamesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi ili kuhakikisha Oktoba 29, 2025 kura zinapigwa kwa amani na CCM inaibuka na ushindi kwa wagombea wake wote.

Timu ya kampeni imethibitisha kuwa kufikia leo, wamefanikiwa kufika vijiji 60 kati ya 68 vilivyomo katika jimbo la Musoma Vijijini, wakipokea mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.



Prev Post Waziri Mchengerwa Ataka Mabadiliko Ya Haraka Huduma Ya Usafiri Jiji La Dar
Next Post Rais Mwinyi Azindua Jumuiya ya Wakandarasi wa Sekta ya Ujenzi Zanzibar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook