Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mgombea Urais Dkt. Samia Aahidi Kuimarisha Madini na Upatikanaji wa Maji Mbogwe, Geita

  • 3
Scroll Down To Discover

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi safari yake ya kampeni kwa kuwasalimia wananchi wa Mkoa wa Geita leo Jumapili.

Akihutubia wananchi katika Viwanja vya Masumbwe, Wilaya ya Mbogwe, Dkt. Samia ameahidi kuanzisha utafiti mkubwa wa kitaifa ili kubaini maeneo mapya yenye madini nchini, sambamba na kuanzisha mchakato wa kuyavuna. Utafiti huu, alisema, utatoa kipaumbele maalum kwa vijana wa Kitanzania katika shughuli za uchimbaji, hivyo kuongeza ajira na fursa za maendeleo kwa vizazi vipya.

“Kwa sasa Tanzania imepimwa kwa asilimia 16 pekee. Lengo letu ni kubaini aina za madini zilizopo katika maeneo mengine ndani ya miaka mitano ijayo,” alisema Dkt. Samia.

Aliongeza kuwa hatua hii itasaidia kuongeza wigo wa uchimbaji wa madini katika Wilaya ya Mbogwe, mkoa ulipewa hadhi ya mkoa wa kimadini, ili kusogeza huduma za madini karibu zaidi na wananchi.

Mbali na madini, Dkt. Samia ameahidi kuendeleza huduma za maji safi katika Wilaya ya Mbogwe. Kwa sasa, kiwango cha upatikanaji wa maji ni asilimia 86, lakini mradi wa maji katika Mji Mdogo wa Masumbwe umekamilika kwa asilimia 68, ukiwa na gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 4.3.

“Kukamilika kwa mradi huu kutaondoa kero ya upatikanaji wa maji katika Kata za Bunigonzi, Mbogwe, Ushirika, Ilolangulu, Isebya, Ngemo na Cikobe, ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za maji hasa wakati wa msimu wa kiangazi,” alisema Dkt. Samia.

Ziara hii ya kampeni ni sehemu ya muendelezo wa CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo Dkt. Samia anaendelea kusisitiza umuhimu wa maendeleo, ajira kwa vijana, na huduma bora kwa wananchi.



Prev Post Polisi Arusha Washikilia Watu 5 Kufuatia Mauaji ya Askari Omary Mnandi – Video
Next Post Mashabiki Wapagawa Na Ngoma Mpya Ya Diamond Platnumz – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook