Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Maelfu Wamiminika Kumsikiliza Dkt. Samia Mbogwe, Geita

  • 4
Scroll Down To Discover

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wa kata ya Masumbwe mara baada ya kuwahutubia katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, Mbogwe mkoani Geita tarehe 12 Oktoba, 2025.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 12 Oktoba 2025, ameendelea na ziara yake ya kampeni katika Mkoa wa Geita, akifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika kata ya Masumbwe, wilayani Mbogwe.

Baada ya kuhutubia umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani, Dkt. Samia alipungia mkono wananchi kwa furaha kama ishara ya shukrani kwa mapokezi makubwa na hamasa waliyoonyesha.

Katika hotuba yake, Dkt. Samia alisisitiza dhamira ya CCM kuendeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, ikiwemo miundombinu ya barabara, elimu, afya na maji safi. Pia aliahidi kuendeleza jitihada za kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta za kilimo, madini, na biashara ndogo ndogo.

Wananchi wa Masumbwe walionekana na hamasa kubwa, wakipeperusha bendera za kijani na njano huku wakipiga nderemo na vifijo wakimsikiliza kiongozi huyo wa taifa.

Ziara hii ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo Dkt. Samia ameendelea kusisitiza amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kisiasa.

#BREAKING: WAGOMBEA UDIWANI 7 wa CCM WATENGULIWA na TUME ya UCHAGUZI – SABABU ZATAJWA…



Prev Post Manka Chuga Azua Gumzo Mitandaoni Kwa Kunywa Vinywaji Vikali Kwa Wakati Mmoja, Afunguka Mazito – Video
Next Post Polisi Arusha Washikilia Watu 5 Kufuatia Mauaji ya Askari Omary Mnandi – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook