Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Familia Yalia Baada ya Kutupiwa Vyombo Nje Nyumba Yao Jijini Dodoma – Video

  • 3
Scroll Down To Discover

Mwanadada Josephine Mosha, amesimulia kisa cha kuhuzunisha cha jinsi familia yao ilivyotupiwa vyombo nje kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi, kisa kikiwa ni mgogoro ambao hauwahusu.

Josephine ameiambia Global TV kwamba walinunua nyumba hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma kwa shilingi milioni 65 ambapo waliandikishana na muuzaji na kupewa nyaraka zote muhimu.

Amezidi kueleza kuwa, wiki chache zilizopita, alifika mwanamke kwenye nyumba hiyo na kujitambulisha kwamba yeye ni mke wa aliyewauzia nyumba na kwamba walikuwa na kesi mahakamani kuhusu talaka, akataka na yeye apewe mgao wake wa kuuza nyumba.

Baada ya kushindwa kufikiana muafaka na mwanamke huyo, ndipo jana wakiwa kwenye shughuli zao, walipopigiwa simu kwamba watu wamevamia nyumba yao wakiwa na silaha na kutoa vyombo nje.



Prev Post Majaliwa: Rais Dkt. Samia Yupo Tayari Kufanya Mambo Makubwa Kwa Wenye Ulemavu
Next Post Manka Chuga Azua Gumzo Mitandaoni Kwa Kunywa Vinywaji Vikali Kwa Wakati Mmoja, Afunguka Mazito – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook