Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

ILI UCHEZE SIMBA YA PANTEV BILA HAYA SAHAU…..

  • 16
Scroll Down To Discover

KOCHA wa Simba Dimitar Pantev, ameleta utaratibu mpya kwenye kikosi hicho, akisema kuwa anataka kufanya kazi na wachezaji wachache, wanaojituma na wenye nidhamu.

Simba kwa sasa ipo kambini ikijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini ya nchini Uswatini, ikiwa ni hatua ya pili ya mtoano ya michuano hiyo mikubwa Afrika baada ya kuvuka kwenye hatua ile ya kwanza.

Timu hiyo inayoongoza Ligi Kuu Bara kwa sasa ikiwa na pointi sita na mabao sita, iliachana na aliyekuwa kocha wake Fadlu Davids ambaye amejiunga na Wydad Casablanca ya Morocco baada ya mchezo miwili ya mashindano msimu huu, Ngao ya Jamii ambayo Simba ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga na mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, ambao Simba ilishinda bao 1-0.

Patev ambaye ni kocha wa zamani wa Gaborone, juzi alisimamia mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Al Hilal na timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka kwenye benchi la ufundi la Simba, kocha huyo ameweka utaratibu mpya kwenye kikosi hicho, lakini kubwa zaidi akisema kuwa anataka kufanya kazi na kundi la wachezaji wachache ambao wanasikilizana, wanajituma na wana nidhamu nje na ndani ya uwanja.

Imeelezwa kuwa ameshawaambia wachezaji kuwa anataka kila mmoja afuate maelekezo na kufanyia kazi yale ambayo kocha atakuwa ameyatoa mazoezini na tangu anakuja Simba hakuwahi kuelezwa kuwa timu hiyo ina kikosi cha kwanza, hivyo kila mmoja ana nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake kwa kuwa kwa sasa kinachoweza kumbeba mchezaji ni uwezo wake tu na siyo historia.

“Kocha nafikiri ameshazungumza na uongozi, anataka kufanya kazi na wachezaji wachache, naona kuna ambao anaweza kuueleza uongozi kuwa wanatakiwa kupelekwa kwa mkopo au kuuzwa ikifika Januari, anasema akiwa na wachache wanajituma zaidi pia inakuwa rahisi kwa benchi lake kuwafuatilia kuliko kuwa na wachezaji 30.

“Lakini pia ameshasema kuwa hakuna mchezaji mkubwa klabuni, kila mmoja anatakiwa kufuata utaratibu unavyotaka, kila mmoja anatakiwa kuwasikiliza waalimu na hadi sasa hana kikosi cha kwanza, yule atakayepata nafasi kwenye mchezo ujao atakuwa amefanya vizuri mazoezini na siyo vinginevyo kwa kuwa anachotaka yeye ni ubora wa mchezaji na siyo historia ya nyuma,” kilisema chanzo hicho.

Mbali na hayo inaelezwa kuwa kocha huyo pia anataka kumtumia mshambuliaji mmoja tu mwenye uwezo mzuri wa kukaa na mpira, lakini anatumia mabeki wanne, viungo wawili wakabaji na viungo watatu washambuliaji, huku akitaka timu yake ianze kutengeneza mashambulizi kuanzia nyuma kwa kipa.

“Anataka timu inayocheza zaidi, kama kuna mtu aliona mchezo dhidi ya Al Hilal anaweza kukueleza jambo hilo, timu inacheza na anataka yafungwe mabao mengi, amekuwa akilalamika sana mchezaji akibutua, inaonekana siyo jambo ambalo analitaka na anasisitiza kipa ndiye aanzishe mashambulizi ya timu.”

Simba itaondoka Jumatano kuelekea Eswatini kuvaana na Nsingizini mchezo utakaopigwa Agosti 18, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mashindano wa kocha huyo raia wa Bulgaria.

The post ILI UCHEZE SIMBA YA PANTEV BILA HAYA SAHAU….. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post HAYA HAPA MAMBO 6 YA KWANZA ‘RORO’ AKITUA YANGA….UZURI NA UDHAIFU WAKE HUU HAPA…
Next Post IBENGE ALIOMBEA MUDA ‘PISHI LAKE’ AZAM FC….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook