

Kufikisha mwishoni mwa kongamano baada ya uwasilishaji na mjadala, wanakongamano wametoa michango ifuatayo:

1. Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi una nafasi muhimu katika kuchochea maendeleo ya nchi na kufikia malengo ya Dira 2050;
2. Ubia kati ya Sekta ya umma na Binafsi unakusudiwa kuipunguzia mzigo serikali ili ijikite zaidi katika maeneo ya huduma za jamii ambazo hazivutii sekta binafsi;
3. Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi sio uuzaji au ubinafsishaji bali ni mashikirikiano ya pamoja ambayo yanaweza kufikia tamati pale inapobidi;
4. Ubia unaiondolea serikali shinikizo la kukopa ili kutekeleza miradi mbalimbali badala yake sekta binafsi inashiriki kufadhili miradi muhimu kupitia ubia;
5. Yapo maeneo mengi hadi ngazi za halimashauri ambayo badala ya serikali kuwekeza moja kwa moja sekta binafsi inaweza ikafanya kwa ushirikiano na serikali. Mfano ujenzi wa maegesho au masoko;
6. Elimu ni nyenzo muhimu katika kufanikisha Dira 2050 lakini inahitaji ushirikiano wa karibu (ubia) kati ya sekta ya umma na sekta ya binafsi;
7. Mabadiliko ya mtaala wa elimu kutoka ule unaoegemea katika maarifa hadi ule wa umahiri, ni nyenzo mwafaka katika kufikia malengo ya Dira 2050, Ijapokuwa uwekezaji mkubwa unahitajika katika kuwajengea uwezo walimu watekeleze kwa ufanisi mtaala mpya;
8. Elimu inayotolewa lazima iweke pia mkazo mkubwa sana katika kufanikishaau kujenga maadili na thamani miongoni mwa wanafunzi ili kufikia vema malengo ya Dira 2050.
9. Kuna haja ya kuboresha zaidi mkakati wa mawasiliano ili miradi ya PPP sio tu iweze kueleweka vema kwa watu wote bali iwe jumuishi kwa makundi yote ili kufikia kwa vitendo malengo ya Dira 2050
10. Dira 2020 inamatumaini ya kushughulikia changamoto za vijana ikiwa ni pamoja na suala la ajira;
11. Ili kufikia malengo ya Dira2050 kuna umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria, umoja wa kitaifa, ushirikishaji, kupambana na rushwa, na kushirikisha serikali za mtaa.
12. Uchumi jumuishi sio tu ni ule unaowasaidia wengi bali pia unatoa fursa kwa wengi kushiriki katika uchumi.
Asilimia kubwa ya Watanzania wanategemea kilimo. Hivyo, ili ulete uchimi jumuishi ni lazima kuongeza tija katika kilimo. Tunatambua hatua kubwa iliyopigwa katika kilimo. Hivyo, miundombinu ya umwagiliaji inapaswa kuongezeka.Dira 2050, inajielekeza kwa hakika kufanikisha Uchumi jumuishi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!