Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Nchimbi Aitikisa Nyamwage Rufiji Akiomba Kura za Dkt. Samia

  • 10
Scroll Down To Discover

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwasili Uwanja wa Soko la Tasaf, katika kata ya Nyamwage, Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, kwa ajili ya Kuendelea na Mikutano ya Kampeni za Urais Kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano ya Oktoba 29 mwaka huu.
Mkoa wa Pwani unakuwa wa 21 kwa mgombea mwenza huyo wa Dkt Samia Suluhu Hassan, wakipeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa Nyamwage Dkt Nchimbi atanadi ilani ya Uchaguzi ya CCM na sera zinazolenga kuwaletea maendeleo Wananchi wote.

Dkt Nchimbi atamwombea kura za urais, Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM.
Mgombea mwenza, Dkt Nchimbi atafanya mikutano Jimbo la Rufiji, Jimbo la Kibiti na Jimbo la Mkuranga.









Prev Post Shangwe na nderemo, kwa matumaini ya kuisha kwa vita Gaza, katika Dira ya Dunia TV
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 10, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook