Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makonda: Dkt. Samia Ni Mwanamke Wa Kwanza Kusababisha Kuwa Na Umeme Wa Uhakika

  • 7
Scroll Down To Discover

Mgombe Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Ndugu. Paul Makonda.

Mgombe Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Ndugu. Paul Makonda, amewaeleza Wananchi wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla juu ya upekee kwa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. katika uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa la Tanzania.

Ndg. Makonda ameeleza kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya kimakati ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla yake iliyogusa moja kwa moja maendeleo ya jamii kwa ujumla wake na kupelekea kuongeza tija ya ukuaji wa kiuchumi.

Katika maelezo yake mbele ya maelfu ya wananchi wa Nyamagana mkoani Mwanza katika muendelezo wa mikutano ya kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. Samia, Makonda amepiga nondo katika utelelezaji wa miradi ya umeme ambapo amegusia mradi wa Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydropower Station (Stiegler’s Gorge)) ambapo amesema mradi huo mkubwa wa umeme wa maji uliojengwa kwenye mto Rufiji, Tanzania una uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme na umeongeza uzalishaji wa umeme nchini.

Aidha, Makonda amesema kupitia mradi huo, Dkt. Samia amelenga kupunguza utegemezi wa umeme kutoka vyanzo vya nje, kuboresha huduma za umeme kwa wananchi na viwanda pamoja na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi jambo ambalo limeanza kuonesha matokea chanya.

Vilevile, Makonda amewataka Watanzania kuendelea kuwa na imani na Dkt. Samia kupitia CCM na kuhakikisha Oktoba 29 kwa pamoja wanashiriki kupiga kura kumchagua Dkt. Samia kuendelea kuongoza Taifa letu katika nafasi ya Urais.



Prev Post Mshtuko! Mwanaume Adaiwa Kumuua Mama Yake wa Kambo
Next Post Nigeria: Waziri Wa Sayansi Ajiuzulu Baada Ya Kughushi Vyeti
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook