Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Shigongo Aomba Barabara na Umeme Buchosa kwa Rais Samia

  • 8
Scroll Down To Discover

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amemuomba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka wananchi wa Wilaya ya Sengerema, hususan Jimbo la Buchosa, katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami akisema ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili wakazi wa eneo hilo wakati wa usafiri.

Aidha, Shigongo alitaja pia tatizo la uhaba wa umeme kuwa changamoto nyingine inayowakwamisha wananchi katika shughuli zao za kiuchumi.

Shigongo aliyasema hayo leo katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika katika Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by globalpublishers (@globaltvonline)



Prev Post Mashindano ya Drafti Tarafa ya Nyaishozi Yalivyonoga
Next Post Sengerema Yazizima Kijani! Wananchi Wamiminika Kumsikiliza Dkt. Samia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook