
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Oktoba 1, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi, Kimara jijini Dar es Salaam kujionea hali ilivyo kituoni hapo.
Akiwa kituoni hapo, Chalamila ametoa ufafanuzi kwa kuwaomba radhi wananchi na kuwaahidi kwamba tayari hatua za dharura zimechukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuhamisha mabasi mapya ili kuyaleta kwenye Barabara ya Morogoro kupunguza tatizo lililopo.
Ameahidi kwamba muda wowote kuanzia kesho, mabasi mapya yataanza kufanya kazi na kuwataka wananchi kuacha hasira za muda mfupi, akieleza kuwa wakati mabasi hayo yanaanza, watu wengi waliyabeza.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!