
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Septemba 30, 2025 ni mgeni rasmi katika mkutano wa kumi na moja wa wadau wa lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa APC uliyopo Bunju jijini Dar es Salaam
Mkutano huo ni jukwaa linalounganisha wadau wote wa lishe kujadili hatua zilizofikiwa, changamoto zilizopo na namna bora ya kuimarisha jitihada za pamoja katika kupambana na utapiamlo na kukuza afya za watanzania.
Pia, Mkutano huo unalenga kujadili na kuimarisha utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22-2025/26)
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!