Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

FIFA Yaiadhibu Afrika Kusini kwa Kumchezesha Mchezaji Asiye na Sifa

  • 2
Scroll Down To Discover

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imetoa adhabu kwa Chama cha Soka cha Afrika Kusini (SAFA) baada ya kubainika kumchezesha Teboho Mokoena, mchezaji asiye na sifa za kushiriki, katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Lesotho uliochezwa mwezi Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Afrika Kusini imenyang’anywa ushindi wake na sasa itaorodheshwa kupoteza mchezo huo kwa mabao 3-0. Aidha, SAFA imelazimika kulipa faini ya CHF 10,000 (takribani shilingi milioni 29 za Kitanzania) kwa FIFA.

FIFA imeipa SAFA siku 10 kuanzia tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huu ili kukata rufaa endapo itaridhika kwamba uamuzi huo si sahihi.

Adhabu hii ni pigo kubwa kwa Afrika Kusini, kwani inaweza kuathiri nafasi yake kwenye mbio za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.



Prev Post Dk.Mwinyi Aahidi Kujenga Masoko Mapya 5 Zanzibar
Next Post Mkurugenzi wa FBI Awataka Watu Kutoombeleza Kifo cha Mama Mlezi wa Tupac
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook