
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeiagiza CHADEMA kukabidhi nyaraka muhimu za kiofisi kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, na wenzake wawili, zitakazotumika kwenye marejeo ya hoja katika kesi ya madai inayohusu madai ya chama hicho kuitenga Zanzibar.
Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatatu Septemba 29, 2025, na Jaji Hamidu Mwanga, anayesikiliza kesi ya madai namba 8323/2025 iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed na wenzake.
Nyaraka ambazo CHADEMA imetakiwa kuwasilisha ndani ya siku 14 ni:
Tamko la mali za chama,
Taarifa za fedha za Benki ya NBC (NBC Bank statements),
Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
Nyaraka zote zikihusu kipindi cha 2019 hadi 2024.
Akizungumza na wanahabari baada ya uamuzi huo, Wakili Hekima Mwasipu alisema kuwa waleta maombi wamepewa siku tisa (9) za kazi kupitia nyaraka hizo, kabla ya Mahakama kuendelea na usikilizaji wa kesi hiyo mnamo Oktoba 30, 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!