Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

AICC Yaendelea Kuboresha kumbi Zake, Yawakaribisha Wadau wa Kitaifa na Kimataifa

  • 5
Scroll Down To Discover

KITUO cha Kimataifa cha Mikutano (AICC)kimesema kuwa  kinaendelea kuboresha kumbi zake mbalimbali huku kikiwakaribisha  wadau  wa kimataifa na kitaifa kufanya shughuli zao za mikutano katika kumbi zao kutokana na madhari uwepo wa madhari nzuri.
Akizungumza leo Septemba 26,2025 wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya 22 ya wahandisi yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mlimani City,Ofisa Mawasilino na Uhusiano,Mourine Kaaya  amesema katika kuendesha mikutano mbalimbali katika kumbi zao ikiwemo Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) imekuwa mstari wa mbele katika kutoa  mchango wake mkubwa wa kuongeza pato la taifa.
Amesema licha ya wao kufaidika lakini na wananchi wanaoishi katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha wamekuwa wakinufaika na uwepo wa kumbi hizo kutokana na kuwaongezea kipato.
“AICC imekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa,pia kwa wananchi  mmoja mmoja kutokana na wageni wanaokuja kwenye kumbi hizi na kufanya mikutano  uhitaji sehemu za kulala,Usafiri na Chakula wakati mwingine.
“Hii ni hatua kubwa kwa  AICC  katika kupata mafanikio yake na sio kwa AICC tu bali kwa taifa kwa ujumla katika kuongezea Pato la nchi,”amesema Kaaya.
Kaaya amesisitiza kuwa  kumbi ya  AICC hina kumbi za mikutano pekee bali zina kumbi nyingine ndogo ndogo za kawaida kwaajili ya Sherehe mbali mbali kama harusi na hafla nyingine.
“Tunawakaribisha wadau wote kwa huduma za kukodi kumbi zetu kwani hatujihusishi na mikutano ya kimataifa tu bali tunajumuisha na mikutano ya ndani ya kawaida,”amesisitiza



Prev Post Shambulio Kanisa Michigan: Watu 4 Wauawa, 8 Wamejeruhiwa – Video
Next Post Nilikuwa Napoteza Kila Wiki EPL, Lakini Hatua Niliyopiga Ilinifanya Ninishinde Jackpot Ya Mamilioni
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook