Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia ampongeza Simbu kwa ushindi wa Dunia, Amkabidhi Nyumba jijini Dodoma

  • 2
Scroll Down To Discover

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha Alphonse Simbu kwa kuwa Bingwa wa Dunia wa mbio za marathon za Tokyo na kwamba ataendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya michezo ili itoe mchango zaidi katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza wigo wa upatikanaji ajira kwa vijana

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jumamosi (Septemba 27, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla kuwapongeza wanamichezo na timu zilizofanya vizuri kwenye medani za kimataifa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa alitangaza kuwa, Rais. Dkt. Samia amempatia Mwanariadha Simbu zawadi ya nyumba jijini Dodoma, sambamba na kikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 ikiwa ni ishara ya kutambua ushindi huo ambao umeliletea Taifa heshima kwenye jukwaa la kimataifa”

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameandaa nyumba iliyopo mkoani Dodoma, ambayo itakabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na zoezi hilo lisichukue muda mrefu kuanzia leo, tusiwe tunatamka ahadi za viongozi halafu zinakaa muda ambao mtu anajiuliza”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Mwanariadha Simbu ameandika ukurasa wa upekee kwa kuwa mtanzania wa Kwanza kutwaa tuzo ya dhahabu katika marathoni ya Dunia ya mwaka 2025 “Haya ni Mashindano makubwa zaidi ya riadha duniani baada ya Michezo ya Olympic, yakihusisha wanariadha Bora kutoka Mataifa yote duniani”

Amesema kuwa Serikali mara zote umekuwa ikiweka jitihada za kutosha za kuhakikisha sekta ya Michezo inakuwa na mchango kwa Taifa “Matokeo tunayoyashuhudia hivi sasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ikiwemo ukarabati WA viwanja na kuongezwa kwa bajeti kutoka shilingi bilioni 38 mwaka 2022 Hadi bilioni 326 mwaka 2025/2026”

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wanamichezo nchini kuweka jitihada binafsi katika kushiriki katika michezo kwani ushindi unaweza kupatikana kwa kuweka.

MKUU wa MKOA wa KILIMANJARO KWENYE UTIAJI SAINI MIRADI MIKUBWA ya KIMIKAKATI…



Prev Post Mgombea Ubunge Buchosa Asisitiza Kuthamini Rasilimali Za Nchi – Video
Next Post JENISTA MUHAGAMA AKIJUMUIKA NA WANA PERAMIHO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook