

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja limesema litawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria watakaofanya vitendo vya ufunjifu wa Amani katika sherehe za Sikukuu ya EID EL FITRI.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Mahonda, Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) ABDULLAH KHAMIS VUAI amesema, Jeshi hilo limejipanga kuimarisha Ulinzi katika maeneo yote ikiwemo nyumba za Ibada, fukwe za bahari na viwanja vya kufurahishia watoto.
Aidha, amewataka madereva wa vyombo vya moto kutii na kuzingatia Sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha majeruhi na vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!