Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Gianni Infantino Asimama Na Amani, Ataka Ulimwengu Kuwaunganisha Watu Kupitia Kandanda

  • 2
Scroll Down To Discover

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, ametoa wito wa amani duniani, akisisitiza haja ya kulinda utu wa binadamu hasa kwa watoto na kina mama wanaoteseka kutokana na vita na migogoro.

Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Infantino alisema:

“Sote tunajua kwamba tunaishi katika ulimwengu uliogawanyika, ulimwengu mkali, ulimwengu mgumu. Na kama ninyi nyote, ninateseka ninapoona watoto wakiteseka na akina mama wakilia.”

Katika mjadala huo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliomba FIFA na UEFA kuchukua hatua kali dhidi ya Israel kwa kuisimamisha kushiriki mashindano ya kimataifa ya kandanda, wakisema ni jibu la lazima kutokana na kile walichokiita “mauaji ya kimbari yanayoendelea katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.”

Hatua hii inakuja wakati migogoro katika Sudan, Gaza na maeneo mengine yenye mizozo duniani ikiendelea kuleta athari kubwa kwa raia wasio na hatia.



Prev Post Mwili wa Hayati, Askofu Mkuu Novatus Rugambwa Umeagwa Roma – Italia
Next Post Rais Mstaafu wa Ufaransa Ahukumiwa Miaka Mitano Gerezani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook