Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TBL Yazindua Ripoti Yake ya Maendeleo Endelevu kwa Mwaka 2025

  • 5
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam, Septemba 2025; Katika moja ya matukio yaliyosubiriwa kwa hamu mwaka huu, Kampuni ya Tanzania Breweries Plc (TBL), ambayo ni kampuni tanzu ys AB InBev na kampuni kinara kwenye utengenezaji na usambazaji wabia nchini, imezindua Ripoti yake ya Uendelevu ya mwaka 2024 jijini Dar es Salaam tarehe 23 Septemba, chini ya kauli mbiu Kua, Tengeneza na Dumisha.

Ripoti hiyo inathibitisha dhamira ya dhati TBL katika kufanya biashara kwa kufuata misingi ya uwajibikaji, kulinda mazingira na kuleta athari chanya kwenye kijamii.

Pia ripoti hiyo imeonesha hatua za makusudi zilizochukuliwa na TBL katika kupunguza uzalishaji utakaoharibu mazingira, kukuza matumizi ya nishati mbadala, kuhifadhi maji, kuwaendeleza wakulima wa ndani na kuimarisha ustawi wa wafanyakazi.

Ripoti hiyo ya mwaka mmoja, inatoa tathmini pana kuhusu maendeleo ya TBL katika sekta ya maendeleo endelevu na ikiwa ni sehemu ya kukamilisha Ripoti ya Mwaka ya Kimataifa ya Anheuser-Busch InBev ya 2024, lengo ni kuonesha dhamira ya dhati ya TBL katika kukuza uwajibikaji na kujenga jamii imara kwa vizazi vijavyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Peter Huyghebaert, aliipongeza TBL kwa kuzingatia miiko ya uwajibikaji na uongozi bora katika shughuli zake. Alisema:

“Kwa muda mrefu TBL imejijengea heshima barani Afrika kutokana na ubora, ubunifu na uwajibikaji wake. Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, imekuwa mfano wa kuigwa si Tanzania pekee bali hata nje ya nchi, ikionesha ni kwa namna gani kampuni inaweza kuchangia maendeleo ya taifa, kuboresha maisha ya watu na kupambana na changamoto kubwa inayokumba dunia ya sasa ambayo ni mabadiliko ya tabianchi.” 

Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Michelle Kilpin, alisisitiza kuwa kampuni hiyo ina wajibu wa kutunza rasilimali kwa vizazi vijavyo, akieleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya TBL imesimamia ukaguzi wa matumizi ya maji, kupunguza moshi unaochafua hewa kwenye mnyororo wa usambazaji na kuzingatia matumizi ya vifungashio vinavyoweza kurejelewa, sambamba na mkakati wa kidunia wa AB InBev wa kupunguza hewa ya ukaa.”

Alisema: “TBL imeendelea kuwa  kampuni kinara kwenye utengenezaji wa bia Tanzania, lakini zaidi ya kutengeneza na kuuza bia, tunaelewa kuwa biashara yetu inategemea mazingira na jamii zinazotuzunguka. Ripoti tunayoizindua leo inasimulia hadithi ya jinsi tunavyosimamia wajibu huo kikamilifu. Kinachotutofautisha si urithi wetu pekee bali pia uwezo wetu wa kuoanisha desturi na mabadiliko ya kisasa.”

Mambo Muhimu katika Ripoti ya 2025

  • TBL ilifikia kiwango cha ufanisi wa matumizi ya maji cha 2.73 hl/hl katika shughuli zake huku zaidi ya asilimia 92 ya bidhaa zake zikitengenezwa kwa kutumia vifungashio vinavyoweza kurejelewa au kutumika tena.
  • Kampuni ilishirikiana na zaidi ya wakulima 2,500 kutoka Kanda ya Kati na Kaskazini mwa Tanzania, wote wakiwa wamepewa msaada wa kifedha na kupewa huduma za ugani wa kilimo ili kuwasaidia waweze kutumia mbinu endelevu xza kilimo na kuhakikisha wanapata kipato cha kudumu.
  • Ukiachana na kilimo, TBL iliwaunga mkono wafanyabiashara zaidi ya 25,000 kwa kuwapa elimu ya fedha, ushauri na vifaa vya teknolojia, jambo lililosaidia kukuza biashara zao.
  • Pia kampuni ilihakikisha kuwa TBL inakuwa ni sehemu ya kazi ambayo ni salama na inayofuata misingi ya haki kwa wafanyakazi wote, ambapo hakuna kifo kilichoripotiwa mwaka 2024 kutokana na kufuata viwango vya usalama, mafunzo ya mara kwa mara na ukaguzi.
  • Kupitia kampeni yake yenye mafanikio makubwa ya kuhamasisha unywaji wa kistaarabu ya Enjoy Like a Boss kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu, TBL iliwafikia mamilioni ya Watanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ikihamasisha unywaji wa kiasi, uwajibikaji na usalama barabarani.



Prev Post Je, Bobi Wine atatoboa katika azma yake ya kuwa rais nchini Uganda? Katika Dira ya Dunia TV
Next Post Dkt. Nchimbi Alivyohitimisha Kampeni Zake Mkoa wa Njombe
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook