Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tshisekedi: DRC Haitauza Rasilimali kwa Bei Rahisi kwa Marekani

  • 3
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, ametangaza kuwa licha ya msaada wa Marekani katika upatanisho wa migogoro, nchi yake haitauza kwa bei rahisi au kupiga mnada rasilimali zake kwa taifa hilo la Magharibi.

Serikali ya Rais Donald Trump imedai kuwa eti na hamu ya kumaliza mapigano ya umwagaji damu mashariki mwa DRC. Aidha Trump ametangaza kuwa atawekeza mabilioni ya dola katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa DRC, huku tarehe ya mwisho ya utekelezaji wa makubaliano hayo ikipangwa mwezi huu.

Rais Tshisekedi ameshiria mwelekeo huo wa Marekani na kusema: serikali yaek itashirikiana katika kuendeleza sekta ya madini na kujenga miundombinu.

Aidha, alibainisha kuwa DRC tayari imesaini ushirikiano wa kimkakati na China, na kwa sasa inaendelea na mazungumzo ya kufikia makubaliano kama hayo na Marekani.

Hata hivyo, Tshisekedi amesisitiza kuwa makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani kati ya Rwanda na DRC, yaliyotiwa saini tarehe 27 Juni, hayajafaulu kupunguza mapigano mashariki mwa Kongo.

Nchi ya Kongo hususan mashariki mwa nchi hiyo, imejaa madini na utajiri mkubwa wa kimaumbile ambao unakodolewa macho na nchi mbalimbali kwa miongo kadhaa, na suala hilo linahesabiwa kuwa moja ya sababu za vita vya sasa mashariki mwa nchi hiyo.

STORI NA ELVAN SITAMBULI | GPL

KAMANDA wa POLISI KINONDONI ATANGAZA KIAMA MABAUNSA WALIOMVAMIA MJANE ALICE – UCHUNGUZI wa HARAKA..



Prev Post Mahakama Kuu Kusikiliza Kesi ya Mpina dhidi ya Tume ya Uchaguzi Septemba 29
Next Post VODACOM TANZANIA PLC PAMOJA NA CHAMA CHA GOFU TANZANIA WAUNGANA ILI KUUNGA MKONO MCHEZO WA GOFU NCHINI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook