Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia Ahidi Mradi wa Umeme na Barabara Kuboresha Maisha ya Wananchi Masasi

  • 2
Scroll Down To Discover

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Ndanda, Masasi mkoani Mtwara katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, tarehe 24 Septemba, 2025.

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango wa kujengwa kwa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ruvuma–Tunduru hadi Masasi mkoani Mtwara, ili kuongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati hiyo katika mkoa huo.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Boma mjini Masasi leo Jumanne Septemba 23, 2025, Dkt. Samia amesema ujenzi huo utahusisha pia vituo viwili vya kupooza na kusambaza umeme, vitakavyohudumia wananchi na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuandaa mazingira ya ujenzi wa kongani za viwanda wilayani Masasi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi mkoani humo.

Katika hotuba hiyo, Dkt. Samia amezungumzia pia miundombinu ya usafiri, akiahidi kuwa iwapo atachaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, serikali itakamilisha ujenzi wa kipande cha barabara ya Mlivata–Mitesa chenye urefu wa kilomita 100, sehemu ya barabara kuu ya Mlivata–Newala–Masasi, kwa kiwango cha lami.

Aidha, ameahidi kuendeleza ujenzi wa barabara za ndani ya mji wa Masasi chini ya usimamizi wa TARURA, ambazo zitajengwa kwa viwango vya changarawe na lami kulingana na mahitaji.

Masista wa Mtakatifu Benedicto wa Msaada wa Kikristo Afrika kutoka Ndanda wakimuombea Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuhutubia wananchi wa Ndanda, Masasi mkoani Mtwara katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, tarehe 24 Septemba, 2025.

 



Prev Post Kikwete Akutana na Bill Gates Katika Hafla ya Goalkeepers New York
Next Post Mwakilishi Wa Mfanyabiashara Amlipua Mjane Alice “Nyumba Iliuzwa 2011 Aliridhia Kwa Dole Gumba”- Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook