Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump Aandaa Mkutano na Viongozi wa Kiarabu Kujadili kadhia ya Ghaza

  • 6
Scroll Down To Discover

Marekani Donald Trump

Msemaji wa ikulu ya White House Karoline Leavitt ametangaza kuwa rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kufanya mkutano na viongozi nchi za Kiarabu na Kiislamu kujadili kadhia ya Ghaza.

Ikimnukuu Leavitt, tovuti ya habari ya Axios imesema, Trump atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Saudi Arabia, Muungano wa Falme za Kiarabu, UAE, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia na Pakistan.

Ikimnukuu mtu mwenye uelewa wa kadhia hiyo, Axios imeongeza kuwa, Trump atawasilisha kwa jopo la nchi hizo pendekezo la mpango wa amani na mfumo wa utawala wa baada ya vita huko Ghaza.

Tovuti hiyo ya habari imebainisha kuwa, mbali na suala la kuwachiliwa huru mateka na kukomeshwa vita, Trump anatarajiwa kujadili mipango ya Marekani kuhusiana na kuondoka jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel na utawala utakaoiendesha Ghaza baada ya vita bila ya kusihirikisha harakati ya ukombozi wa Palestina ya Hamas.

STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 24 , 2025
Next Post Jinsi ya Kujua Kiasi cha Maji Kinachofaa kwa Mwili Wako, Soma Hapa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook