Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

HIZI HAPA TAMU & CHUNGU ZA FADLU NDANI YA SIKU 444 ZA FADLU AKIWA NA SIMBA…

  • 1
Scroll Down To Discover

KOCHA wa Simba Fadlu Davids ametafuta njia yake mpya, baada ya kuamua kuikimbia timu hiyo akirejea Morocco ambako wakati wowote atatangazwa kuwa kocha mpya wa Raja Athletic ya huko.

Fadlu ameshtua umma wa timu hiyo baada ya kubadili gia angani ikiwa ni siku chache tangu atoke kuwatangazia zaidi ya mashabiki 60,000 kwamba msimu huu ni maalum kwa ajili ya mafanikio baada ya kuwa hapo kwenye msimu uliopita wakijenga msingi wa kutenegeneza timu imara.

Ukianzia kuhesabu kuanzia jana Septemba 22,2025 maana yake ni kwamba Fadlu amefikisha siku 444 ndani ya Simba kuanzia Julai 5, 2024 alipotangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

Fadlu kuondoka Simba, zipo alama tofauti ambazo kocha huyo anaziacha ndani ya Simba na hata nje ya klabu hiyo ambazo zitabeba jina lake au wakati mwingine kubaki kama deni nyuma yake.

BENCHI LENYE UTULIVU

HABARI ZA SIMBA- FADLUMuda ambao Fadlu amekaa ndani ya Simba, mambo yalionekana kutulia kuanzia kwenye benchi lake na hata kikosi cha timu hiyo, aliingiza utamaduni mkubwa wa weledi idara ya ufundi.

Ilikuwa rahisi kuona Fadlu anamfokea mchezaji uwanjani lakini ilikuwa ni njia ya kutaka kuona mambo yanafanikiwa na sio chuki binafsi kisha baada ya mchezo maisha ya amani na furaha yalikuwa yanaendelea.

Hili lilikuwa tofauti na baadhi ya watangulizi wake ambao kulikuwa na kuibuka na migingano mbalimbali kati ya kocha na wachezaji wake, hatua ambayo iliwaondolea wachezaji kujiamini.

SIMBA IMARA

Habari za Simba leoMsimu wake wa kwanza, Fadlu aliiongoza vyema Simba ikiukosa ubingwa kwenye mchezo wa mwisho baada ya kufungwa na Yanga walioibuka mabingwa.

Kama mchezo ule usingechezwa, alikuwa analibeba taji hilo la ubingwa, kikubwa ni kwamba aliitengeneza Simba imara uwanjani, ilikuwa na njaa ya ushindi muda wote wa dakika 90 kiasi cha kuikimbiza Yanga vizuri.

FAINALI CAF

Habari za Simba leoKuifikisha Simba fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ilikuwa ni jambo kubwa zaidi katika msimu wake huo wa kwanza katika timu hiyo.

Kumbuka msimu huo Simba wakati wanampa Fadlu timu, lengo ilikuwa ni angalau ifike hatua ya nusu fainali baada ya wekundu hao kukwamia sana katika hatua ya robo fainali.

Fadlu aliivusha Simba hapo na akafanya zaidi kwa kuipeleka fainali kabisa na ishu ngumu ikawa ileile kwamba ubora ukaamua tena apoteze taji, badala ya Yanga na huko akakutana na RS Berkane ambayo ni wazi ilikuwa kubwa zaidi ya wekundu hao.

Hii ilikuwa ni fainali ya kwanza ya Afrika kwa Simba katika mfumo wa sasa tangu ilipocheza fainali ya Kombe la CAF 1993, na hivyo kuipa heshima kubwa klabu hiyo lakini pia kwake ikamjengea jina kubwa zaidi kwenye CV yake sokoni.

SIMBA MOYONI

Habari za Simba leoSimba ilionekana kuanza kumkaa moyoni Fadlu na pengine ndio maana kila alipokuwa akishinda mechi ngumu alikuwa anajikuta anashindwa kujizuia na kujikuta analia kama ambavyo alikuwa anafanya ilipofuzu nusu fainali na hata fainali ya CAF.

Hapa ndani kwenye zile mechi ngumu aliwahi kuonekana akigawa fedha mithili ya pedezyee kwa mashabiki ambao walikuwa wamezidiwa na furaha na kuamua kukimbia na gari aliyokuwa anapanda huku akigusa upande wa moyo wake na nembo ya klabu hiyo.

MZEE WA PAMBA

Habari za Simba- Fadlu DavidsFadlu ukiacha kuipenda kazi yake, mwenyewe alikuwa anajipenda sana. Uwanjani kwenye mechi akiwa utamuona kwenye fulana maalum za klabu au utamuona ndani ya vazi la suti na raba zake.

Alijiweka tofauti na makocha wengine ambao walishindwa kujitengenezea mwaonekano tofauti. Katika moja ya mahojiano  alisema jukumu la kusimamia unadhifu wake liko kwa mke wake.

HANA KOMBE

Ndani ya muda ambao Fadlu amefanya kazi nchini akiwa na Simba medali kubwa aliyowahi kuivaa ni kuwa mshindi wa pili, akiipata kwenye ligi msimu uliopita, fainali ya shirikiho na msimu huu akiwa mshindi wa pili kwenye Ngao ya Jamii. Hakufanikiwa kupata taji lolote la ubingwa akiwa na wekundu hao.

TATIZO YANGA, SINGIDA

HABARI ZA SIMBA-FADLUKukwama kwa Fadlu kuchukua mataji ya ndani mchawi wa kwanza ni mtani wa Simba ambaye ni Yanga. Fadlu msimu uliopita kwenye ligi alipoteza mechi mbili tu na zote ilikuwa dhidi ya Yanga, hakuna timu nyingine iliondoka na pointi tatu mbele ya wekundu hao kwenye ligi.

Katika Kombe la Shirikisho (FA) hapa mchawi akabadilika badala ya Yanga ikawa Singida Black Stars ambayo iliiondosha Simba kwenye hatua ya nusu fainali kwa kipigo cha mabao 3-1 na kuifanya timu hiyo kukosa taji la pili.

YANGA KUMBUKUMBU MBAYA ZAIDI

Fadlu mpaka anaondoka Simba hakuwahi kupata ushindi muhimu dhidi ya Yanga ambao kisiasa ni hatua mbaya baina ya timu hizo mbili.

Timu nyingi zimefungwa chini ya Fadlu lakini hadi anaondoka, Yanga ilimsumbua na kupoteza mechi zote nne walizokutana akishindwa kuifunga angalau bao hata moja.

KIBOKO YA VIGOGO

Msimu huu wakati Simba ipo kwenye dirisha la uhamisho, taarifa zinasema usajili ulikuwa unafanyika chini ya watu wachache msimamizi mkuu akiwa ni yeye, akifanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu, Mohammed ‘Mo’ Dewji.

Hili halikupita kirahisi hasa baada ya baadhi ya vigogo kuwekwa kando, hivyo kujikuta akikosa sapoti kutoka kwa baadhi ya vigogo ambao walikuwa wanamtegea kusubiri kuona atakwamia wapi.

Kusajili timu nzima bila ya vigogo kuingilia sio jambo jepesi katika soka la Bongo na hiyo ikatajwa kama mwanzo wa kujinunulia tiketi ya mapema ya kuianza safari ya kuondoka Msimbazi.

Kila la kheri Fadlu!

Credit:- MwanaSpoti.

The post HIZI HAPA TAMU & CHUNGU ZA FADLU NDANI YA SIKU 444 ZA FADLU AKIWA NA SIMBA… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BAADA YA KUANZA KINYONGE CAF….WASAUZI WA SIMBA WAFUNGUKA YA MOYONI….
Next Post Kwa nini Ufaransa na Uingereza wamelitambua taifa la Palestina? Katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook