

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema hana sababu ya kuyakwepa mazungumzo na Marekani kama nchi hiyo haitomshinikiza kuachana na silaha za Nyuklia.
Akizungumza katika hotuba yake mbele ya bunge Kim alisisitiza kuwa kamwe hatoachana na silaha hizo ili nchi yake indolewe vikwazo.
Kim Jong Un ameongeza kuwa iwapo Marekaniitaachana na mpango wake wa kuitaka nchi yake iachana na silaha zake za nyuklia na kukubali hali iliyopo sasa na kutaka makubaliano ya kweli ya amani ya kushirikiana pamoja basi haoni sababu ya nchi yake kutokaa chini na Marekani na kuelewana.
Kauli ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini imetolewa wakati serikali ya Korea Kusini ikitoa wito kwa Rais wa Marekani Donald Trump azungumze na Kim miaka sita baada ya mazungumzo yote ya amani kuvunjika. Majadiliano ya kipindi cha nyuma na serikali ya Pyongyang yalisitishwa kutokana na vikwazo na kutakiwa iachane na silaha za nyuklia.
Rachel Minyoung Lee mtaalamu wa masuala ya Korea Kaskazini katika taasisi moja ya Marekani, amesema hii ni mara ya kwanza kwa Kim kutaja jina la Trump hadharani tangu alipoapishwa na kuingia rasmi madarakani Januari 20.
Amesema hii ni njia mojawapo ya Kim kumtaka Trump kufikia upya sera ya Marekani ya uondoaji wa silaha za nyuklia, kwamba iwapo nayo Marekani itajiondoa katika sekta hiyo basi Korea Kaskazini inaweza kukaa chini na kuzungumza na taifa hilo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!