
Taharuki kubwa imeibuka Mikocheni jijini Dar es Salaam, baada ya mjane Alice Haule kuvamiwa na watu kwenye nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mumewe, Justice Rugaibula kisha kumtoa kwa nguvu pamoja na wapangaji wenye asili ya Kichina, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.
Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu mumewe, alikopa fedha kutoka kwa mfanyabiashara mmoja, kiasi kinachotajwa kuwa ni shilingi milioni 150, ambapo alianza kurejesha lakini kabla hajamaliza, akafikwa na umauti.
Mvutano huo ukapelekwa mahakamani ambapo inadaiwa kuwa kabla ya muafaka kufikiwa, ndipo walipokuja kutolewa kwenye nyumba yao.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!