

Mwanamama Shakira Arsenal, mkazi wa Upanga, Dar es Salaam, anaomba msaada wa hali na mali ili kuikomboa nyumba aliyonunua kwa ajili ya watoto wake mwaka 2018, kabla ya kuingia katika ndoa na raia wa Canada, Farid, mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Shakira, mwaka 2021 akiwa nchini Canada, mume wake alimtumia talaka kupitia WhatsApp na kumtaka alipe gharama zote alizotumia wakati wa ndoa yao. Aidha, Farid anataka nyumba hiyo iuzwe na mgawanyo wa asilimia 50/50 ufanyike, jambo ambalo Shakira anapinga kwa kuwa alilinunua kabla ya ndoa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!