
Dodoma, Juni 24, 2025 – Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026 yenye jumla ya shilingi trilioni 56.49, baada ya mjadala wa siku saba.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, akisoma matokeo ya kura za kupitisha bajeti hiyo, amesema kuwa kati ya Wabunge 392 waliotarajiwa kushiriki, 378 walihudhuria, huku 13 wakiwa hawakuwepo na nafasi moja ikiwa wazi.
Kati ya waliopiga kura:
378 walipiga kura za ndiyo,
Kura za hapana: 0,
Kura 5 hazikuwa na uamuzi,
Hii inaifanya bajeti hiyo kupita kwa asilimia 98.7, ikionesha uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wabunge.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!