Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Harmonize Aibua Gumzo na Kionjo cha ‘Best Couple’

  • 40
Scroll Down To Discover

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, ameibua mjadala mitandaoni baada ya kuachia kionjo cha wimbo wake mpya Best Couple kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika kionjo hicho, Harmonize alionyesha cover art ya wimbo huo inayomwonyesha akiwa na mrembo Kajala – hali iliyoibua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki wake.

Wengi wameonekana kumpongeza kwa ubunifu na ujasiri wa kuendelea kuonyesha ukaribu wake na Kajala, huku wengine wakidai huenda wawili hao wameamua kurudiana au kuweka wazi mahusiano yao kwa mara nyingine.

Ingawa Harmonize hajathibitisha rasmi kama Kajala ndiye anayeongelewa kwenye wimbo huo, mashabiki wameendelea kuhusisha jina lake na ujio wa Best Couple, wakisema ni kama “mwendelezo wa penzi lililosimama.”



Prev Post Rwanda na DRC Wakubali Amani, Trump Ajisifu Bila Kutambuliwa Rasmi
Next Post MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 22 June 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook