Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kikwete Awasilisha Ripoti ya Migogoro kwa Rais wa Malawi

  • 12
Scroll Down To Discover

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) (Panel of Elders, POE) akiwa katika picha ya pamoja na Profesa Arthur Peter Mutharika, Rais wa Malawi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, baada ya kufanya naye mazungumzo jana Ijumaa jijini Lilongwe, Malawi.

Pamoja nao ni Mama Joyce Banda, Rais Mstaafu wa Malawi, ambaye ni Mjumbe wa Jopo hilo la Wazee. Katika mazungumzo yao, pamoja na mambo mengine, Viongozi hao walipata fursa ya kumweleza Rais Mutharika kuhusu kazi zilizofanywa na zinazoeandelea kufanywa na POE katika kusuluhisha migogoro katika nchi za Ufalme wa Lesotho, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na kwa sasa Madagascar.

Kimuundo, POE ni moja ya vyombo vya kuzuia migogoro na kurejesha amani katika nchi za SADC ambacho kinaripoti moja kwa moja kwenye Asasi ya SADC Troika, ambayo nchi ya Malawi ndiyo Mwenyekiti wake kwa sasa.

 

The post Kikwete Awasilisha Ripoti ya Migogoro kwa Rais wa Malawi appeared first on Global Publishers.



Prev Post ‘Bwege’ Afariki Dunia Akiwa Hospitalini Kigamboni
Next Post Trump Atishia Kuchukua Mafuta Iran na Kuteka Kisiwa cha Kharg – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook