Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Aggy Baby Afichua Ukweli! Asema Poshqueeen Hajaolewa, Ile Ilikuwa Kiki Tu!

  • 31
Scroll Down To Discover

Mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii, Poshy Queen

MSANII wa Bongo Muvi, Agness Suleiman Kihamba maarufu kama Aggy Baby ameendelea kusisitiza kuwa mrembo wa mitandaoni Poshqueeen hajaolewa, akidai tukio lililozua gumzo mitandaoni lilikuwa kiki ya kutangaza upya SPA yake.

Aggy amesema kuwa SPA hiyo imekuwepo kwa muda mrefu, lakini haikufanya vizuri mwanzoni, hivyo wameamua kuihuisha kwa mbwembwe na kutumia tukio la “ndoa” kama njia ya kukuza umaarufu wa biashara hiyo.

MSANII wa Bongo Muvi, Agness Suleiman Kihamba maarufu kama Aggy Baby

“Unajua mimi niliongea waziwazi nikasema jamani hakuna harusi pale. Nyie wenyewe mmejionea, hiyo ndoa iko wapi? Mimi nikiongeaga watu wananionaga naroho mbaya au chuki, lakini mimi naongeaga vitu vya ukweli,” alisema Aggy Baby kwa msisitizo.

Kauli hiyo imezua mjadala mpya mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea Poshqueeen wakisema hakuna ubaya kutumia ubunifu wa kibiashara, na wengine wakidai imezidi kuvuka mipaka ya ukweli.

Kwa sasa, Poshqueeen bado hajazungumza moja kwa moja kujibu madai hayo, huku mashabiki wakingojea kauli yake rasmi.

VIDEO: TAZAMA TUNDU LISSU ALIVYOLETWA MAHAKAMANI KESI YAKE UHAINI INAUNGURUMA LEO..



Prev Post Donald Trump Aongoza Orodha ya Wagombea Tuzo ya Amani ya Nobel
Next Post Diddy Ampiga Simu Trump – Aomba Msamaha Baada ya Kifungo cha Miezi 50!
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook