Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Diamond Afuta Ujumbe wa Kuoa Mke wa Pili, Mashabiki Washangaa

  • 60
Scroll Down To Discover

Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz.

Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, ameibua maswali mapya mitandaoni baada ya kukanusha taarifa za kuoa mke wa pili, kisha ghafla kufuta ujumbe huo muda mfupi baadaye.

Awali, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliandika maneno mazito:

“Naona kuna misumari inapigiliwa kuwa Simba kaongeza mke, hapana jamani sijaongeza, msinipe ujasiri nisiokuwa nao.”

Mtangazaji wa Wasafi Aaliyah anadaiwa kuolewa mke wa pili na Diamond Platnumz.

Lakini kabla mashabiki hawajamaliza kusherehekea au kuhoji zaidi, ujumbe huo ukatoweka. Hatua hiyo imezua gumzo jipya, baadhi wakidai huenda ni mkakati wa kutengeneza kiki kuelekea kuachia kazi mpya, huku wengine wakihisi huenda staa huyo ana kitu kizito anachokificha.

Licha ya sintofahamu hiyo, Diamond amesisitiza kwamba mwezi huu ni wa burudani na raha pekee, akiahidi mashabiki wake video mpya ambazo zipo njiani kuachiwa.

VIJANA ZAIDI 100 WAIPA KAMPUNI ya ULINZI SIKU 7 – UDANGANYIFU WATAJWA – BOSI wa KAMPUNI AKIRI….



Prev Post Vigogo CHADEMA Waburuzwa Mahakamani, Wamo John Heche na Mnyika
Next Post Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awasili Malawi Kumwakilisha Rais Samia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook