Muuguzi wa India asubiri kunyongwa Julai 16

Nimisha Priya Na mwandishi wetu, Elvan Stambuli Nimisha Priya alihukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanamume mmoja ambaye alikuwa mshirika wake wa zamani wa kibiashara, Talal Abdo Mahdi – ambaye mwili wake uliokatwakatwa uligunduliwa kwenye tanki la maji mnamo 2017. Njia pekee ya kumuokoa muuguzi huyo ni kama familia ya Mahdi itamsamehe. Ndugu na wafuasi wake wametoa $1m (£735,000) kama diyah, au pesa ya damu, ili kulipwa kwa familia ya Mahdi. “Bado tunasubiri msamaha wao au matakwa mengine,” mjumbe wa shirika linalomtetea aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC. “Tarehe ya kunyongwa ( Julai 16 mwaka huu) imewasilishwa na mkurugenzi mkuu wa mashtaka kwa mamlaka ya jela. Bado tunajaribu kumwokoa. Lakini hatimaye familia inabidi ikubali kumsamehe,” Babu John, mwanaharakati wa masuala ya kijamii na mjumbe wa shirikamoja linalopigania kumuokoa nesi huyo alisema. Afisa katika wizara ya mambo ya nje ya India aliiambia BBC kwamba bado wanajaribu kuthibitisha maelezo hayo. Nimisha Priya alikuwa ameondoka katika jimbo la kusini mwa India la Kerala kwenda Yemen mwaka 2008 kufanya kazi ya uuguzi. Alikamatwa mwaka wa 2017 baada ya mwili wa Mahdi kugunduliwa. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa amefungwa katika jela kuu ya Sanaa katika mji mkuu wa Yemen. Alishtakiwa kwa kumuua Mahdi kwa kumpa “kiwango cha juu cha dawa za kumtuliza” na kudaiwa kuukatakata mwili wake baada ya kufariki dunia. Hata hivyo, Nimisha alikanusha madai hayo. Mahakamani, wakili wake alidai kwamba Mahdi alimtesa kimwili, akampokonya pesa zake zote, akamnyang’anya pasipoti yake ya kusafiria na hata kumtishia kwa bunduki. Muuguzi huyo alisema alijaribu kumpa dawa ya ganzi Mahdi ili tu kuchukua pasipoti yake kutoka kwake, lakini dozi iliongezeka kwa bahati mbaya. Mnamo 2020, mahakama ya eneo hilo ilimhukumu kifo. Familia yake ilipinga uamuzi huo katika Mahakama ya Juu ya Yemen, lakini rufaa yao ilikataliwa mwaka wa 2023. Mapema Januari mwaka huu, Mahdi al-Mashat, rais wa Baraza Kuu la Wahouthi, aliidhinisha kunyongwa kwake. Mfumo wa mahakama wa Kiislamu wa Yemen, unaojulikana kama Sharia, unampa matumaini ya mwisho – kupata msamaha kutoka kwa familia ya mwathirika kwa kulipa pesa za damu.

KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU….

BAADA ya kucheza dakika 11 kwenye mechi mbili za Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Manchester City na Juventus, kiungo mshambuliaji wa Wydad, Stephane Aziz KI huenda asiwe sehemu ya kikosi hicho msimu ujao huku ikielezwa ili abaki kuna ishu anaisikilizia. Wydad ilicheza mechi tatu za michuano hiyo na kuondolewa hatua ya makundi bila ushindi ikianza na kichapo cha mabao 2-0 kutoka Man City ambapo Aziz KI alicheza kwa dakika saba, Juventus iliwachapa 4-1 Aziz KI akicheza dakika nne na ililala 2-1 dhidi ya Al Ain huku Aziz KI akiwa hakucheza kabisa mchezo huo wa mwisho. Mchango wake ndani ya klabu hiyo bado haujaonekana kwa kiwango kilichotarajiwa huku kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu akitanguliwa na Thembinkosi Lorch na Nordin Amrabat ambao wanacheza nafasi moja uwanjani. Lorch ambaye alicheza mechi zote tatu za Kombe la Dunia la Klabu akifunga bao moja, ndiye anayetajwa kushikilia hatma ya Aziz KI kwani Msauzi huyo anacheza hapo kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns. Mkataba huo wa mkopo unamalizika Julai 31, 2025 huku kukiwa na ripoti kwamba Wydad imeridhishwa na uwezo wake, hivyo inatak kumsajili moja kwa moja. Kwa mujibu wa jarida la Kiarabu la Al-Botola, Aziz KI anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa kigeni wanaoweza kuachwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Hii ni kutokana na shinikizo la kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni hadi watano ili kutokukiuka kanuni za Ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro 1), wakati sasa Wydad wana jumla ya wachezaji 11 wa kigeni, hivyo kocha Mohamed Benhachem ametakiwa kuwasilisha majina ya wachezaji wa kupunguza ili wabaki watano. Ikiwa Wydad watakamilisha usajili wa Lorch kama inavyodaiwa, basi nafasi ya Aziz KI itazidi kuwa finyu, hali inayoweza kumfanya aondoke labuni hapo mapema kuliko ilivyotarajiwa. “Usajili wa Aziz KI una vificho vingi hadi sasa ukiniuliza alisaini mkataba wa muda gani siwezi kukupa jibu kwani haijajulikana kutokana na Wydad kushindwa kuweka wazi tofauti na Mwalimu (Selemani) ilivyokuwa, lakini ninachofahamu ni kwamba kocha hajaridhishwa na uwezo wa kiungo huyo anaweza akaondoshwa kikosini,” kilisema chanzo cha taarifa hiyo. “Wakati baadhi ya vyanzo vikizungumza nyota huyo alisajiliwa kwa mkopo akitokea Yanga kukiwa na kipengele cha kumnunua na kuna vyombo vingine vinaripoti alisaini mkataba wa miaka mitatu, hivyo hii ni shida.” Wakati ikielezwa hivyo, kwa mujibu wa Transfermarkt – tovuti inayojihusisha na soka ikiwemo usajili wa wachezaji, Aziz KI alisaini mkataba wa miaka miwili Wydad unaomalizika Juni 2027. Kuhusu suala la Mtanzania Mwalimu, chanzo kilidai huenda akarudishwa timu ya vijana moja kwa moja kwa ajili ya kuendelea kukuza uwezo tofauti na awali ilivyokuwa ambapo alikuwa anapata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa. Awali, ilielezwa Aziz KI aliyeitumikia Yanga kwa misimu mitatu tangu Julai 2022 akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast ameuzwa Wydad kwa Sh2 bilioni. Aziz KI alitambulishwa na Wydad Mei 24, 2025 sambamba na nyota wengine wawili wapya waliojiunga kujiandaa na michuano ya Kombe la Dunia la Klabu inayoendelea nchini Marekani. Wachezaji wa kigeni waliopo Wydad ni mabeki wa kati Guilherme Ferreira (Brazil) na Bart Meijers (Uholanzi), kiungo mkabaji Mickal Malsa (Ufaransa), viungo washambuliaji Arthur Wenderroscky (Brazil), Pedrinho (Brazil), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) na Thembinkosi Lorch (Afrika Kusini). Wengine ni washambuliaji Omar Al-Somah (Syria), Samuel Obeng (Ghana), Seleman Mwalimu (Tanzania) na Cassius Mailula (Afrika Kusini) anayecheza kwa mkopo akitokea Toronto FC ambapo mkataba wake huo unatarajiwa kumalizika Agosti 1, 2025. WASIKIE YANGA Wakati sintofahamu ikiwa kubwa juu ya hatma ya Aziz KI ndani ya Wydad, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kiungo huyo alipelekwa huko kwa mkopo. “Mkataba ambao Aziz KI aliusaini na Wydad wakati tunamuuza ni wenye vipengele viwili – miezi mitatu ya kwanza wanamuangalia, wakijiridhisha na kiwango watamuongeza kwa miaka miwili,” alisema Kamwe. Alisema kwa mujibu wa makubaliano, Julai 10, mwaka huu Wydad wanatakiwa kuwasiliana na Yanga juu ya ishu ya Aziz KI kuendelea kusalia huko. “Aziz Ki bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga. Endapo watashindwana naye basi atarejea nchini na atakuwepo kwenye mchezo wetu wa kwanza wa kufungua msimu ujao kwenye Ngao ya Jamii.” The post KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU…. appeared first on Soka La Bongo.

DIB YAENDELEA KUELIMISHA UMMA KUHUSU MAJUKUMU YAKE KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Pamoja na kuzungumza na wananchi wanaotembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB) katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea, Meneja Uendeshaji wa DIB, Bw. Nkanwa Magina, alipata fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari kwa lengo la kuuhabarisha umma mkubwa zaidi majukumu ya DIB. Mwananchi aliyetembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB), akioneshwa kauli mbiu ya DIB inayosema Tunakinga Amana Yako katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.  Afisa Mwandamizi wa DIB, Bw. Silvan Makole, akisisitiza jambo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Diamond Platnumz x Masterpiece YVK ft Xman RSA & Lintonto - Down. (Official )

Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA

FESTAC ‘77’ kuwakilisha sekta ya sinema Afrika Cannes 2025 Na Mwandishi Wetu Kama unapenda filamu zenye mizizi ya kihistoria, zenye maana ya kina, na zinazotangaza utambulisho wa Kiafrika – basi hii ni habari njema: FESTAC ‘77, filamu inayosubiriwa kwa hamu, imechaguliwa na Shirika la Filamu la Nigeria (NFC) kwa onyesho maalum katika Tamasha la Filamu la Cannes 2025! Filamu hii ya kipekee, iliyotayarishwa na Adonis Production na kusambazwa na FilmOne Entertainment, inatupeleka nyuma hadi mwaka 1977 – kwenye tukio la kihistoria la Tamasha la Pili la Dunia la Sanaa na Utamaduni wa Watu Weusi na Waafrika (FESTAC) lililofanyika Lagos, Nigeria. FESTAC ‘77 si tu filamu ya burudani. Ni kazi ya sanaa inayotambua na kusherehekea urithi wa kitamaduni wa Afrika. Kupitia simulizi lililojaa hisia na maelezo ya kihistoria yaliyochambuliwa kwa kina, filamu hii inafufua tukio ambalo lilikutanisha wasanii, wanazuoni, na wanaharakati kutoka pande zote za dunia ya watu weusi – wote kwa lengo moja: kudai nafasi ya Afrika katika utamaduni wa dunia. Na sasa, filamu hii inapanda jukwaa kubwa kabisa la kimataifa – Cannes Film Festival, ikiwakilisha Afrika kwa fahari. Adonijah Owiriwa, Mtay“Filamu hii ni urejeshaji wa historia tajiri ya Afrika. Ni njia ya kutuonesha sisi wenyewe – ndoto zetu, changamoto tulizokutana nazo, na mafanikio yetu. Kupitia sinema, tunadhibiti simulizi letu na kuhakikisha dunia inatusikiliza kwa sauti yetu wenyewe.” Kwa upande wake, Kene Okwuosa, Mkurugenzi Mtendaji wa Filmhouse Group, anaona uteuzi huu kama ushindi wa hadithi za Kiafrika:  “Kwa muda mrefu, simulizi za Afrika zimewekwa pembeni au kuwasilishwa kwa njia potofu. FESTAC ‘77 ni ishara ya mabadiliko. Tunaingia kwenye zama mpya ambapo hadithi zetu zinapewa nafasi inayostahili kwenye majukwaa ya dunia.” Kwa Prince Tonye Princewill, ambaye pia ni Mtayarishaji Mkuu wa filamu, FESTAC ‘77 ni kielelezo cha maendeleo makubwa katika ubora na uwezo wa sinema ya Afrika:  “Afrika haipo tena pembezoni mwa tasnia ya filamu. Tumejipanga, tumekomaa, na sasa tunashindana kimataifa. Filamu hii si tu hadithi, bali ni ushahidi wa uwezo wa Kiafrika katika utayarishaji wa filamu zenye kiwango cha juu.” Filamu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwaka 2025. Lakini kabla ya hapo, watazamaji wa Cannes watakuwa wa kwanza kuiona. FESTAC ‘77 inachukua hadithi ya zamani ya bara letu na kuileta kwa ladha mpya – ikiunganisha historia na sanaa ya sasa, na kuipa dunia nafasi ya kuona Afrika kwa macho mapya. Hii ni zaidi ya filamu – ni mwamko wa kiutamaduni. Ni Afrika ikijiandika upya. Na huu ni mwanzo tu.

TNC Musik – Deka

Muuguzi wa India asubiri kunyongwa Julai 16

KUHUSU ISHU YA AZIZ KI KUTAKIWA KUTEMWA WYDAD…..YANGA WAWAPA JIBU HILI WAARABU….

DIB YAENDELEA KUELIMISHA UMMA KUHUSU MAJUKUMU YAKE KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Diamond Platnumz x Masterpiece YVK ft Xman RSA & Lintonto - Down. (Official )

ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA

Muziki

Don't miss daily Music

Total Views: 158,464
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook