Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Biteko: Rais Samia Anapenda Kufanya Kazi Na Viongozi Wa Dini

  • 46
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko

Dodoma, Julai 3, 2025 – Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuongoza nchi kwa misingi ya maridhiano, mazungumzo na ushirikiano na viongozi wa dini katika kulinda na kuendeleza amani ya taifa.

Akizungumza jijini Dodoma, alipomwakilisha Rais Samia katika Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dkt. Biteko amesema Rais Samia ni kiongozi anayefungua milango ya mazungumzo badala ya kutumia mabavu au mamlaka aliyo nayo kikatiba.

“Mheshimiwa Rais Samia anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini, na ninyi ni mashahidi – amekuwa akiwaalika mara kadhaa ili kujadili masuala ya kitaifa. Kama angekuwa mtu wa kujifungia na kusema ‘nina jeshi, nina vyombo vya ulinzi na katiba’, hali ingekuwa ngumu sana,” alisema Dkt. Biteko.

Aliongeza kuwa kwa uongozi wa sasa, Serikali imekuwa wazi na tayari kupokea maoni kutoka kwa viongozi wa dini, hasa pale panapohitajika mwelekeo mpya wa kitaifa katika kujenga mshikamano, amani, na maadili ya taifa.

“Yeye amesema, milango yetu iwe wazi tuzungumze kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu, hasa pale ambapo tunahisi hatuendi sawasawa,” alisisitiza Biteko.

Mkutano huo wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) umejumuisha viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini, ukiwa ni jukwaa la kuimarisha mshikamano kati ya dini na serikali katika maendeleo ya taifa.



Prev Post GEITA: Afisa Mtendaji wa Kijiji na Raia Wenzake Wakamatwa kwa Tuhuma za Mauaji – Video
Next Post Twende Butiama 2025: Vodacom Tanzania na Stanbic Bank zaendelea kutoa matumaini kwa Watanzania
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook