Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

WANANCHI WAKARIBISHWA KUTEMBELEA BANDA LA BODI YA BIMA YA AMANA MAONESHO YA SABASABA 

  • 10
Scroll Down To Discover

Wananchi wamekaribishwa  kutembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana katika maonesho ya sabasaba ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na bodi hiyo 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana Isack Kihwili wakati akizungumza na Fullshangwe kuelezea mabadiliko mbalimbali yanayotarajiwa na bodi Hiyo wakati mchakato wa kisheria utakapokamilika

Bw.Kihwili ameyasema hayo katika banda la bodi hiyo kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Saba Saba yanayoendelea kwenye viwanja wa Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam

Amesema kuwa wanashiriki kwa mara ya kwanza kabisa maonesho ya sabasaba wakiwa wamesimama wao wenyewe ambapo miaka iliyopita walikuwa wanashiriki maonesho hayo wakiwa chini ya benki kuu ya Tanzania kwani walikuwa ni sehemu ya benki kuu lakini hivi sasa wanasimama wenyewe .

Amesema kuwa , wanawakaribisha wananchi kwa ujumla wawe wenye amana au wasiwe na amana waweze kutembelea kwenye banda lao lililopo sabasaba ili waweze kunifunza majukumu.yao pamoja na huduma wanazotoa .

“Tunarudia kusisitiza kuwa jukumu letu kubwa ni kutoa kinga kwa amana za wateja wale ambao wameweka amana zao kwenye benki na taasisi za fedha nchini .”

Amesema kuwa,jukumu.lao ni kutoa kinga kwa kutoa fidia kwa mwenye amana pale ambapo benki yake au taasisi ya fedha alipoweka amana hiyo imefungwa na benki kuu ya Tanzania kwa kukiuka taratibu au kwa kufilisika .

“Tunawakaribisha sana wananchi waweze kujifunza mambo mengi ambayo wanayafanya na namna gani watanufaika na uwepo wa taasisi hiyo .”amesema

“Kama nilivyosema tutakuwa tunasimama wenyewe lakini hiyo yote ni kutokana na maboresho makubwa ambayo yamefanyika kwenye hiyo taasisi .”amesema .

Ameongeza kuwa ,moja ya maboresho ambayo wanayafanya ambayo mengine yanaendelea kwenye mchakato wa kisheria na kiutawala ni pamoja na kutunga sheria ambayo itaweka majukumu ya hiyo taasisi kwa uwazi zaidi na taratibu nyingi za uendeshaji zitawekwa wazi katika hiyo sheria hata muundo wa taasisi umeidhinishwa kwa hiyo taasisi itaongezeka kwa maana ya watumishi na vitengo vile ambavyo vinahudumia watu kwa maana ya maeneo mbalimbali kwa mfano kitengo chao cha mawasilliano nacho kimeundwa hivyo watakuwa na mawasilino ya karibu sana na umma

“Kutakuwa na mawasilino ya karibu sana na wananchi na wataweza kuwasiliana moja kwa.moja tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa wapite benki kuu ili waweze kuwapata ila kwa sasa watawapata moja kwa moja kwa ajili ya kutoa huduma au ushauri kwa mtu yoyote ambaye anafika kwa ajili hiyo.”ameongeza .

“moja ya mambo ambayo tunasisitiza katika maonesho haya ni kuwaomba wananchi husuani wale ambao walikuwa wateja wa benki zile zilizopo katika ufilisi wale ambao hawajachukua malipo ya fidia ya bima ya amana wafanye hivyo kwani pesa hizo zipo.”amesema .

“Tunatoa wito kwa wale watu ambao walikopa katika mabenki ambayo yapo katika ufilisi wafanye hima waweze kulipa kwani madeni yao ili bodi ya bima ya amana iwezekupata nafasi ya kuwalipa wale ambao wandai pesa zao kwani wanashindwa kulipwa kwa ukamilifu kwa sababu pesa zipo nje watu walikopa lakini bado hawajalipa.”amesema .



Prev Post ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA
Next Post NMB YATAMBULISHA ATM MAALUM YA KUWEKA FEDHA KATIKA MAONESHO YA SABASABA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook