Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Juliana Shonza Aibuka Kinara Kura za Maoni za UWT Songwe

  • 38
Scroll Down To Discover

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza ameongoza kwa idadi ya wingi wa kura za maoni baada ya kupigiwa kura na wajumbe kwenye uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani humo.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Bw. Antony Mtaka, amesema Bi. Shonza, amepata jumla ya kura 572, akifuatiwa na Bi. Neema Mwandabila, aliyepata kura 356 ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa huo, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Bi. Tully Magilla aliyepata kura 167.

Uchaguzi huo umehusisha wagombea tisa ambapo kando na hao watatu wengine ni Bi. Tumaini Mbembela, kura 122, Bi. Shukuruni Mkondya kura 86, Bi. Winfrida Shonde kura 56, Bi. Messiah Swela kura 44,Bi. Betha Minga kura 34 na Bi. Neema Lwila kura 29, ambapo jumla ya kura 739 zimepigwa na kura 5 zikiharibika.

 



Prev Post Regina Ndege Aibuka Mshindi Kura za Maoni Viti Maalum CCM Manyara
Next Post SBL Yazindua Mpango Wa Kilimo Biashara Kuongeza Mavuno kwa Wakulima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook