Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Regina Ndege Aibuka Mshindi Kura za Maoni Viti Maalum CCM Manyara

  • 44
Scroll Down To Discover

Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni za Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, Jabir Shekimweri, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, amemtangaza Regina Ndege kuibuka mshindi baada ya kupata kura 891 kati ya zaidi ya kura 1,000 zilizopigwa.

Uchaguzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Manyara, ukihusisha wagombea mbalimbali waliowania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Bunge kupitia nafasi za Viti Maalum kwa wanawake.

Katika nafasi ya pili aliibuka Yustina Rahhi aliyepata kura 703, akiibuka mshindani wa karibu zaidi wa Regina Ndege.

Orodha ya Wagombea Wengine na Kura Zao:

Senorina Yunus – 214

Joyclen Umbulla – 168

Loema Peter – 90

Paulina Nahato – 71

Schola Mollel – 37

Anna Shinini – 23

Wagombea waliopata kura chache sasa wanabaki kusubiri mchakato wa mwisho wa vikao vya juu vya CCM vitakavyopitisha jina la mwisho la mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.



Prev Post Silvia Sigula na Jacqueline Mzindakaya Watinga Ubunge wa Viti Maalum CCM
Next Post Juliana Shonza Aibuka Kinara Kura za Maoni za UWT Songwe
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook