
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini humo NATION, kuwa makubaliano ya maridhiano kati yake na aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta maarufu kama ‘Handshake’ yalilenga mabadiliko ya kitaifa wala haikuwa kwa sababu za kibinafsi au kujifaidisha kisiasa.
“Hakuna mmoja kati ya watu wangu aliyeteuliwa kuwa ndani ya serikali ya Uhuru. Sikupata chochote,” Odinga alisema.
Raila Odinga alizungumzia hilo na kuelezea kwamba aidha, haikuwa suala la nipe nikupa.
“Uhuru alikuwa amemaliza muda wake madarakani. Na akasema kwamba ataniunga mkono na aliniunga mkono. Na hicho pekee ndicho kilichofanyika. Sikuwa na makubaliano yoyote ya kibanafsi na Uhuru”, Odinga aliongeza.
Raila Odinga aliweka wazi kuwa msingi wa maridhiano kati yao, ulikuwa mabadiliko ya katiba juu ya utawala wa kimfumo na masuala ya uchaguzi huku akilaumu mahakama kwa kusambaratika kwa jopo lililojulikana kama Building Bridges Initiative (BBI).
“Tulikubaliana masuala yaliyohitaji mabadiliko chini ya jopo la BBI. Mahakama ndio iliotupilia mbali BBI. Lakini kama ingepitishwa, haingetokea jinsi ilivyokuwa mwaka 2022 kwa sababu BBI ingekuwa imefanya mabadiliko katika taasisi muhimu ikiwa ni pamoja na taasisi ya uchaguzi.
Raila Odinga Airushia Lawama Mahakama Kenya Raila Odinga alisema kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama ambao ulitupilia mbali jopo la BBI, ulifanya asiwe na lakufanya na suala hilo kuwa nje ya uwezo wake.
“Mahakama ndio iliyotuvuruga, sio mimi”, Odinga alisema.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!