
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewasili nchini Belarus kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kukuza fursa za kiuchumi kati ya Tanzania na Belarus.
Mheshimiwa Majaliwa alipokelewa rasmi katika Uwanja wa Ndege wa Kinsk na Naibu Waziri Mkuu wa Belarus, Viktor Karankevich, pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali ya Belarus.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ameambatana na ujumbe wa viongozi wakuu wa serikali akiwemo:
Balozi wa Tanzania nchini Urusi na Belarus, Mhe. Frederick Ibrahim Kibuta
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Mhe. Cosato Chumi
Ziara hii inatarajiwa kujikita katika maeneo ya ushirikiano wa kibiashara, elimu, viwanda, kilimo na teknolojia, sambamba na kusaini mikataba ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Tanzania na Belarus zimeendelea kuimarisha uhusiano wao katika miaka ya hivi karibuni, ambapo Belarus imeonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya kilimo, usafirishaji na teknolojia ya viwanda.
Ziara ya Mheshimiwa Majaliwa inatazamwa kama hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya wananchi wa pande zote.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!