
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Jumanne Mabodo (30) kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wake Kabula Masanja (50) kwa kumkata kwa panga nyumbani kwa marehemu, kijiji cha Chumwi, Wilaya ya Musoma, Julai 19, 2025. Binti wa marehemu, ambaye ni mke wa mtuhumiwa, alijeruhiwa na anaendelea na matibabu. Chanzo ni mgogoro wa kifamilia baada ya mke wa mtuhumiwa kudai kuwa mumewe ni mwizi.
Katika tukio jingine, Marwa Mgesi (17) wa Mugumu Serengeti, alikamatwa na silaha aina ya pisto yenye risasi 4 aliyomwibia bosi wake huko Monduli, Arusha.
Polisi pia wanachunguza kifo cha Nyangige Matiku (44) wa Mtukula, Butiama, aliyedaiwa kujinyonga kutokana na wivu wa mapenzi.
Jeshi la Polisi limewaasa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!