Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Ramaphosa Amfuta Waziri Kontrovershali wa Elimu ya Juu

  • 26
Scroll Down To Discover

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amefanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri kwa kumfuta kazi Waziri wa Elimu ya Juu na Mafunzo ya Kiufundi, Dkt. Nobuhle Nkabane, ambaye amekuwa akikabiliwa na malalamiko na utata kuhusu ufanisi wake katika kusimamia sera za elimu ya juu nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu, mabadiliko hayo yameelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha sekta ya elimu ya juu, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikikumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo utekelezaji wa sera, upatikanaji wa fedha kwa wanafunzi na utawala wa taasisi za elimu.

Nafasi ya Dkt. Nkabane sasa imechukuliwa na Buti Manamela, ambaye ni sura inayofahamika kwa wengi katika sekta hiyo. Manamela aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kuanzia mwaka 2017 hadi 2024, na kabla ya hapo aliwahi kuhudumu kama Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais kati ya 2014 hadi 2017.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa, kurejeshwa kwa Manamela kunatazamwa kama hatua ya kimkakati ya Rais Ramaphosa kurejesha imani ya umma na kuongeza kasi ya mageuzi ndani ya wizara hiyo muhimu.

Aidha, katika hatua nyingine ya kuimarisha uongozi wa wizara hiyo, Rais Ramaphosa amemteua aliyekuwa Waziri Mkuu wa Mkoa wa KwaZulu-Natal, Dkt. Nomusa Dube-Ncube, kuwa Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Mafunzo. Uteuzi wake unaonekana kama sehemu ya mkakati wa kuongeza usimamizi na ufanisi katika wizara hiyo inayoshughulika moja kwa moja na mustakabali wa vijana wa Afrika Kusini.

Mabadiliko haya yanakuja wakati ambapo serikali ya Ramaphosa inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa wanafunzi, wanaharakati na wadau wa elimu waliokuwa wakitaka mabadiliko ya msingi katika mfumo wa elimu ya juu.



Prev Post Tanzania na Belarus Kuimarisha Ushirikiano Kupitia Ziara ya Majaliwa
Next Post Bao Mbili Tu, Ushindi Tayari. Ni Early Payout ya Meridianbet
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook