Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MNASEMA KIBU HAJAWIKA MSIMU HUU 🙄🙄..?HIZI HAPA TAKWIMU ZAKE ZA KUTISHA 😎😎…

  • 45
Scroll Down To Discover

SIMBA SC katika anga la kimataifa msimu wa 2024/25 imegotea nafasi ya pili kwa kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Katika dakika 180, Simba SC ilifungwa jumla ya mabao 3-1, bao la kufutia machozi kwa Simba SC lilifungwa na Joshua Mutale mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Kibu Dennis ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa katika ubora kwenye mashindano ya kimataifa kwa kufunga mabao muhimu katika mechi za ushindani Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika Ligi Kuu Bara 2024/25 haukuwa msimu bora kwa Kibu D kutokana na namba kuwa chini hasa katika eneo la kutengeneza pasi za mwisho.

Kibu D alitoa jumla ya pasi nne na kufunga mabao manne na kasi katika kufunga mabao ilianza kuonekana katika mzunguko wa pili.

Rekodi zinaonyesha kuwa amecheza jumla ya mechi 24 za ligi ya NBC akifunga mabao manne na kutoa pasi nne hivyo kahusika katika mabao 8 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC.

The post MNASEMA KIBU HAJAWIKA MSIMU HUU 🙄🙄..?HIZI HAPA TAKWIMU ZAKE ZA KUTISHA 😎😎… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 10. 2025
Next Post ISHU YA MPANZU KUTAKIWA NA WAARABU …UKWELI WOTE HUU HAPA…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook