Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla Awatakiwa Kila la Heri Gambo na Makonda Kuelekea Katika Uchaguzi

  • 20
Scroll Down To Discover

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema anawatakia kila la kheri Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo ni watoto wa baba na Mama mmoja ambaye ni CCM.

Pia amesema hawezi kuingilia ugomvi uliopo kati ya wawili hao kwani amesema wanachopitia kwa sasa ni kipindi cha mpito na watakaa sawa kikipita kwani wao ni marafiki, hivyo amewatakia heri wawili hao katika mchakato utakaofuata.

Makalla amebainisha hayo leo Juni 6,2025 wakati akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Arusha Mjini mkoani Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tisa katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

“Hawa wote hawa Gambo na Makonda nawatakia kila la heri, wote wananifahamu mimi ni kaka yao na mimi nasimama kila la heri, siwezi kuingilia ugomvi ukishakuwa na wadogo zako unawaacha huu ni mwezi mchanga utapita tu,” amesema Makalla.

Ameongeza: Huu ni muda mdogo kidogo tu na sio hapa tu mengi yanafanyika huko lakini hawa ni watoto wa mama mmoja na baba mmoja Chama Cha Mapinduzi, kwanza ni marafiki kwahiyo muwe makini, hawa ni marafiki wanajuana na mimi namtakia kila mmoja wao heri katika mchakato utakaofata”.



Prev Post MAGAZETI ya Leo Jumamosi 07 June 2025
Next Post Innocent Bashungwa: Tumieni Teknolojia Za Kisasa Kudhibiti Uhalifu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook