Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Marekani yampongeza Rais Mteule wa Korea Kusini

  • 36
Scroll Down To Discover


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amempongeza Rais mpya Mteule wa Korea Kusini Lee Jae-myung na kueleza nia yake ya kufanya kazi na kiongozi huyo wa mrengo wa kati.

Rais mpya wa Korea Kusini Lee Jae-myung anaapishwa katika Bunge la taifa mjini Seoul leo Juni 4, 2025.
Nchi hizo mbili zimeunganishwa na muungano usioweza kuvunjika na Mkataba wa Ulinzi wa Pamoja, maadili na uhusiano wa kina wa kiuchumi, Rubio amesema katika taarifa yake na Marekani ikisalia kuwa mdhamini wa jadi wa usalama wa Korea Kusini.

Mgombea wa kiliberali nchini Korea Kusini, Lee Jae-myung, ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo dhidi ya mpinzani wake wa kihafidhina Kim Moon Soo na ambaye shirika la habari la nchini humo, Yonhap limeripoti kwamba amekubali kushindwa katika uchaguzi huo.
Kulingana na Yonhap, Lee ameshinda kwa asilimia 49.4 ya kura, wakati Kim akipata asilimia 41.1 huku idadi ya wapiga kura ikitajwa kuwa ilikuwa karibu asilimia 80.



Prev Post Marekani yampongeza Rais Mteule wa Korea Kusini
Next Post Marekani yampongeza Rais Mteule wa Korea Kusini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook