Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Donald Trump, Elon Musk waingia kwenye mgogoro mzito – Video

  • 30
Scroll Down To Discover


Katika kile kinachoonekana kuwa mgogoro mpya kati ya watu wawili waliowahi kuwa washirika wa karibu, bilionea wa teknolojia Elon Musk amemkosoa vikali Rais wa Marekani, Donald Trump, kwa kuunga mkono muswada wa bajeti na kodi ambao umeibua mjadala mkubwa nchini humo.
Musk aliuita muswada huo “uchafu wa kuchukiza” (disgusting abomination), huku akionyesha masikitiko na hasira kwa walioupigia kura.

Muswada huo, uliopitishwa na Baraza la Wawakilishi mwezi uliopita, unahusisha upunguzaji mkubwa wa kodi, ongezeko la matumizi ya kijeshi, na kuongezwa kwa kiwango cha madeni ambacho serikali ya Marekani inaweza kukopa. Umetajwa kuwa ajenda kuu ya muhula wa pili wa Trump.

“Aibu kwa walioupigia kura,” Musk aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), katika kauli yake ya kwanza ya hadharani kumpinga Trump tangu aondoke serikalini mnamo Mei 31. Musk alikuwa amejiunga na utawala huo kwa siku 129 chini ya timu yake inayojulikana kama Doge, iliyokuwa ikifanya kazi ya kupunguza matumizi ya serikali.

Katika mfululizo wa machapisho kwenye mtandao wa X, Musk alikosoa vikali muswada huo kwa kusema kuwa utapanua zaidi nakisi ya bajeti hadi kufikia dola trilioni $2.5, hali ambayo itawaumiza raia wa Marekani kwa madeni yasiyoweza kustahimilika.

Katika siasa za Marekani, “pork” ni matumizi ya serikali kwenye miradi inayowanufaisha wabunge binafsi majimboni mwao. Musk, ambaye hapo awali aliapa kufadhili wapinzani wa kisiasa wa Republican watakaoenda kinyume na ajenda ya Trump, sasa anaonya: “Novemba ijayo, tunawafukuza wanasiasa wote waliomsaliti mwananchi wa kawaida.”
Miongoni mwa waliopinga ni Seneta wa Kentucky, Rand Paul, aliyesema hatounga mkono iwapo utapanua deni la taifa. Trump alijibu kwa mfululizo wa machapisho kwenye mitandao ya kijamii, akimuita Paul mtu asiyeelewa lolote na ambaye “watu wa Kentucky hawampendi”.

Kiongozi wa wengi katika Seneti, John Thune, aliwataka Warepublican wasonge mbele na ajenda waliyoiahidi wakati wa kampeni, licha ya “tofauti za maoni”. Spika wa Bunge, Mike Johnson, alimtetea Trump na muswada huo kwa kusema:“Rafiki yangu Elon amekosea sana. Huu ni mwanzo muhimu.”

Inadaiwa pia kuwa kutoridhika kwa Musk kulichochewa na hatua ya serikali kukataa pendekezo lake la kuendesha usimamizi wa anga kwa kutumia mfumo wa Starlink, kutokana na wasiwasi wa mgongano wa maslahi na changamoto za kiteknolojia.

Trump na republicans wanapanga kupitisha muswada huo kabla ya tarehe 4 Julai, huku Musk akiwa ameacha historia ya kutoa zaidi ya dola milioni 250 kwa kampeni ya Trump mwaka jana. Trump pia anapendekeza mpango wa kupunguza matumizi kwa dola bilioni 9.4, kwa misingi ya mapendekezo ya timu ya Doge – ukilenga msaada wa nje, USAID, na taasisi kama NPR na PBS.



Prev Post Duma Boko: Tumaini Jipya la Botswana, Afata Nyayo za Traore – Video
Next Post Donald Trump, Elon Musk waingia kwenye mgogoro mzito – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook