Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Korea Kusini; nchi iliyokuwa ikihesabu umri wa mtoto tangu akiwa tumboni

  • 5
Scroll Down To Discover

Nchi ambayo mtoto anapozaliwa alikuwa anahesabiwa kuwa na mwaka mmoja ni Korea Kusini (na zamani Korea Kaskazini pia ilifuata utaratibu huu). Mfumo huu wa kihistoria unaitwa “Korean age system”, ambapo mtu huhesabiwa kuwa na umri wa mwaka mmoja punde tu anapozaliwa, na kila mtu huongezewa mwaka mmoja tarehe 1 Januari, bila kujali tarehe yao ya kuzaliwa halisi.
Mtoto akizaliwa tarehe 31 Desemba 2024, siku inayofuata (1 Januari 2025), atahesabika kuwa na miaka miwili kwa mujibu wa mfumo huo, ingawa kwa umri wa kimataifa atakuwa na siku moja tu.
Mnamo mwaka 2023, Korea Kusini ilianza kutumia rasmi mfumo wa umri wa kimataifa (ambapo mtu anahesabiwa kuwa na umri wa miaka 0 anapozaliwa na huongezewa mwaka mmoja kila baada ya mwaka mmoja wa kuzaliwa kwake). Hii ni sehemu ya jitihada za kupunguza mkanganyiko wa kimataifa.
Kwa hiyo, kihistoria Korea Kusini ilikuwa inatumia mfumo huo, lakini sasa wamehamia kwenye mfumo wa kimataifa ambao ni wa kawaida duniani kote baada ya kupitishwa sheria kufuta utamaduni huo.
Sheria hiyo imefuta mfumo ule wa jadi uliokuwa ukimhesabu Mkorea kuwa na umri wa mwaka mmoja pindi anapozaliwa, kwa kujumlisha muda aliokaa tumboni mwa mama.
Mabadiliko haya, ambayo sasa yanahesabu umri wa mtu kwa kuzingatia tarehe halisi ya kuzaliwa, yalianza kutekelezwa mwaka 2021.
Rais Yoon Suk Yeol alihamasisha sana mabadiliko haya alipokuwa akiwania urais. Alisema kuwa mbinu hizo za jadi za kuhesabu umri zilileta “gharama zisizo za lazima kijamii na kiuchumi”.
Kwa mfano, migogoro iliibuka kuhusu ulipaji wa bima na uamuzi wa kustahiki kwa baadhi ya programu za msaada wa serikali.
Hapo awali, mfumo uliotumika sana nchini Korea ulikuwa ni ule wa “umri wa Kikorea” ambao umekuwa ukitumika kwa karne nyingi, ambapo mtu huhesabiwa kuwa na mwaka mmoja pindi tu anapozaliwa, na huongezewa mwaka mmoja kila tarehe 1 Januari. Hii inamaanisha kuwa mtoto aliyezaliwa tarehe 31 Desemba atakuwa na umri wa miaka miwili siku inayofuata.
Wabunge walipiga kura kuondoa tamaduni hiyo ya jadi mnamo Desemba mwaka 2023.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya ndani ya Hankook Research mwezi Januari 2022 ulionyesha kuwa watu watatu kati ya wanne wa Korea Kusini waliunga mkono uamuzi huo wa kuoanisha mfumo huo na wa kimataifa.
Mbinu hizi za jadi za kuhesabu umri ziliwahi pia kutumika katika nchi nyingine za Asia Mashariki, lakini nyingi imeziacha.
Japani ilikuwa na utamaduni huo lakini ilianza kutumia kiwango cha kimataifa mwaka 1950, huku Korea Kaskazini ikifuata katika miaka ya 1980.
ENDS



Prev Post Rais Samia Aweka Jiwe La Msingi Makao Makuu Ya Chama Cha Mapinduzi – (Picha +Video)
Next Post Rais Samia Aweka Jiwe La Msingi Makao Makuu Ya Chama Cha Mapinduzi – (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook