Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kituo cha Biashara Ubungo kuifanya Tanzania kitovu cha biashara na usafirishaji Afrika

  • 42
Scroll Down To Discover

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo, Dar es Salaam ni hatua muhimu ya kimkakati inayolenga kutatua changamoto sugu zilizokuwa zikikwamisha biashara na usafirishaji nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Rais Samia amesema kupitia mradi huo, masuala kama vile ucheleweshaji wa mizigo, gharama kubwa za uendeshaji wa biashara, pamoja na ukosefu wa miundombinu rafiki kwa wafanyabiashara, sasa yanakwenda kupatiwa majibu ya kudumu.

“Kutokana na huduma zinazopatikana hapa na urahisi wa kufanya biashara, kutaongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kupunguza muda wa ushughulikiaji wa mizigo kutoka siku saba hadi chini ya siku tatu,” amesema.

Amefafanua kuwa kituo hicho kimewekewa mifumo ya kisasa na ya kidijitali itakayowawezesha wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa. Aidha, ameeleza kuwa jengo hilo linatarajiwa kuwa kiunganishi muhimu cha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na China, huku likihamasisha mauzo ya bidhaa zenye thamani ya juu kwenda masoko ya nje.

Aidha, Rais Samia ametoa rai maalum kwa wazalishaji kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa kwa ajili ya soko la kimataifa zinazingatia viwango vya ubora ili kuiheshimisha nchi.

Mradi huo mkubwa ulianza kutekelezwa mwezi Mei 2023 na hadi sasa umetajwa kugharimu Shilingi bilioni 282.7. Kituo cha EACLC kinatajwa kuwa mojawapo ya miradi ya kimkakati yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara, usindikaji wa mazao, na usafirishaji barani Afrika.

The post Kituo cha Biashara Ubungo kuifanya Tanzania kitovu cha biashara na usafirishaji Afrika appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 02, 2025
Next Post Benki ya Exim Tanzania Yazindua Elite Banking
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook